12-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kumswalia Maiti na Kufuata Jeneza na Kuhudhuria Kuzikwa Kwake na Karaha kwa Wanawake Kufuata Jeneza
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب الصلاة عَلَى الميت وتشييعه وحضور دفنه
وكراهة اتباع النساء الجنائز
12-Mlango Wa Kumswalia Maiti na Kufuata Jeneza na Kuhudhuria Kuzikwa Kwake na Karaha kwa Wanawake Kufuata Jeneza
Hadiyth – 1
عن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ شَهِدَ الجَنَازَةَ حَتَّى يُصَلَّى عَلَيْهَا ، فَلَهُ قِيراطٌ ، وَمَنْ شَهِدَهَا حَتَّى تُدْفَنَ ، فَلَهُ قِيرَاطَانِ )) قِيلَ : وَمَا القِيرَاطانِ ؟ قَالَ : (( مِثْلُ الجَبَلَيْنِ العَظِيمَيْنِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kushuhudia jeneza mpaka likaswaliwa atakuwa na ujira wa Qiraati moja na mwenye kushuhudia mpaka akazikwa maiti, atakuwa na ujira wa Qiraati mbili." Akaulizwa: "Na Qiraati mbili ina maana gani?" Akasema: "Ni mfano wa majabali mawili makubwa." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasai']
Hadiyth – 2
وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنِ اتَّبَعَ جَنَازَةَ مُسْلِمٍ إيماناً وَاحْتِسَاباً ، وَكَانَ مَعَهُ حَتَّى يُصَلَّى عَلَيْهَا وَيُفرَغَ مِنْ دَفْنِهَا ، فَإنَّهُ يَرْجعُ مِنَ الأَجْرِ بِقيراطَيْنِ كُلُّ قِيرَاطٍ مِثْلُ أُحُدٍ ، وَمَنْ صَلَّى عَلَيْهَا ، ثُمَّ رَجَعَ قَبْلَ أنْ تُدْفَنَ ، فَإنَّهُ يَرْجِعُ بِقيرَاطٍ )) رواه البخاري .
Kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kufuata jeneza la Muislamu kwa Imani nakutaraji radhi za Allaah, Atarejea na malipo ya Qiraati mbili, kila Qiraati nikama Mlima wa Uhud, na mwenye kuliswalia, kisha akarudi kabla ya kuzikwa atarudi na Qiraati moja." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 3
وعن أم عطية رضي الله عنها ، قالت : نُهِينَا عَنِ اتِّبَاعِ الجَنَائِزِ ، وَلَمْ يُعْزَمْ عَلَيْنَا . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kwa Ummu Atwiyyah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: "Tumekatazwa kufuata jeneza, na (hilo) halikuazimiwa kwetu sisi." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuwd]