14-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kisomo Katika Swalaah ya Jeneza

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب مَا يقرأ في صلاة الجنازة

14-Mlango Wa Kisomo Katika Swalaah ya Jeneza

 

Alhidaaya.com

 

 

إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ  ﴿٥٦﴾

Hakika Allaah na Malaika Wake wanamswalia Nabiy. [Al-Ahzaab: 56]

 

 

فَإنَّهُ لاَ تَصحُّ صَلاَتُهُ إِذَا اقْتَصَرَ عَلَيْهِ ، ثُمَّ يُكَبِّرُ الثَّالِثَةَ ، وَيَدعُو للمَيِّتِ وَللمُسْلِمِينَ بِمَا سَنَذكُرُهُ مِنَ الأحاديث إنْ شَاءَ اللهُ تَعَالَى ، ثُمَّ يُكَبِّرُ الرَّابِعَةَ وَيَدْعُو . وَمِنْ أحْسَنِهِ : (( اللَّهُمَّ لاَ تَحْرِمْنَا أجْرَهُ ، وَلاَ تَفْتِنَّا بَعدَهُ ، وَاغْفِرْ لَنَا وَلَهُ )) . وَالمُخْتَارُ أنه يُطَوِّلُ الدُّعاء في الرَّابِعَة خلافَ مَا يَعْتَادُهُ أكْثَرُ النَّاس ، لحديث ابن أَبي أَوْفى الذي سَنَذْكُرُهُ إنْ شَاء اللهُ تَعَالَى .

Kwani haisihi Swalaah bila ya kusoma Suratul Faatihah. Kisha ataleta takbira ya tatu, na kumuombea maiti na Waislamu wote kwa jumla kama tutakavyo taja Hadiyth in shaa Allaah. Kisha atapiga tabiri ya nne, na aombe kwa dua tofauti, na zilizo bora ni: Allaahumma laa tahrimna ajrahu walaa taftinna ba'dahu waghfirlana walahu. Na inayopendeza ni aifanye dua ndefu katika takbira ya nne kinyume na walivyozoea watu wengi kwa mujibu wa Hadiyth ya Ibn Abu Awfaa ambayo tutaitaja in shaa Allaah. 

 

 

Hadiyth – 1

عن أَبي عبد الرحمان عوف بن مالك رضي اللهُ عنه ، قَالَ : صَلَّى رسول الله صلى الله عليه وسلم عَلَى جَنازَةٍ ، فَحَفِظْتُ مِنْ دُعَائِهِ ، وَهُوَ يقُولُ : (( اللَّهُمَّ اغْفِرْ لَهُ وَارْحَمْهُ ، وَعَافِهِ وَاعْفُ عَنْهُ ، وَأكْرِمْ نُزُلَهُ ، وَوَسِّعْ مُدْخَلَهُ ، وَاغْسِلْهُ بِالمَاءِ وَالثَّلْجِ وَالبَرَدِ ، وَنَقِّه مِن الخَطَايَا كَمَا نَقَّيْتَ الثَّوْبَ الأَبْيَضَ مِنَ الدَّنَس ، وَأبدلْهُ دَاراً خَيْراً مِنْ دَارِهِ ، وَأهْلاً خَيراً مِنْ أهْلِهِ ، وَزَوْجَاً خَيْراً مِنْ زَوْجِهِ ، وَأدْخِلهُ الجَنَّةَ ، وَأعِذْهُ مِنْ عَذَابِ القَبْرِ ، وَمنْ عَذَابِ النَّارِ )) حَتَّى تَمَنَّيتُ أن أكُون أنَا ذَلِكَ الْمَيِّت . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu 'Abdir-Rahmaan 'Awf bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Alituswalisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Swalaah ya jeneza, nikahifadhi katika dua yake akisema: "Ee Mola mdgufirie na umrehemu, na msalimishe na msamehe, na mkirimu kwa kushuka kwake, na kunjua kuingia kwake. Na muoshe kwa maji, theluji na barafu. Na safisha makosa yake kama inayosafishwa nguo nyeupe kutokana na uchafu. Na mbadilishie nyumba yake, na jamaa bora kuliko nyumba yake, na jamaa bora kuliko jamaa zake. na mwenza kuliko bora kuliko mwenza wake. Na mwepushe na adhabu ya kaburi, na adhabu ya moto. Mpaka nikatamani kuwa niwe huyo maiti." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة وأبي قتادة وَأبي إبراهيم الأشهلي ، عن أبيه – وأبوه صَحَابيٌّ – رضي اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم : أنَّهُ صَلَّى عَلَى جَنَازَةٍ ، فَقَالَ : (( اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِحَيِّنَا وَمَيِّتِنَا ، وَصَغِيرنَا وَكَبيرنَا ، وَذَكَرِنَا وَأُنْثَانَا ، وشَاهِدنَا وَغَائِبِنَا ، اللَّهُمَّ مَنْ أحْيَيْتَهُ مِنَّا فَأحْيِهِ عَلَى الإسْلاَمِ ، وَمَنْ تَوَفَّيْتَهُ مِنَّا فَتَوفَّهُ عَلَى الإيمَان ، اللَّهُمَّ لاَ تَحْرِمْنَا أجْرَهُ ، وَلاَ تَفْتِنَّا بَعدَهُ )) رواه الترمذي

Imepokewa kwake Abu Hurayrah na Abu Qataadah na Abu Ibraahiym Al-Ashhaliyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kutoka kwa babake, na babake ni Swahaaba kutoka Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): kuwa aliswalisha Swalaah ya jeneza, akasema: "Ee Mola wasamehe walio hai miongoni mwetu na waliokufa, na watoto wetu na wazee wetu, na wanaume wetu na wanawake, na waliopo na wasio kuwepo. Ee Mola, yeyote miongoni mwetu utakaye mpatia uhai mfanye aishi juu ya Uislamu na utakaye mfisha miongoni mwetu mfishe katika Imani. Ee Mola usituharamishie ujira wake wala usitufitini baada yake." [At-Tirmidhiy]

 

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( إِذَا صَلَّيْتُمْ عَلَى المَيِّتِ ، فَأخْلِصُوا لَهُ الدُّعاء )) رواه أَبُو داود .

Na amesema Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mnapo mswalia maiti basi ksudieni dua zenu kwa ikhlasi." [Abu Daawuwd]

 

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم في الصَّلاَةِ عَلَى الجَنَازَةِ : (( اللَّهُمَّ أنْتَ رَبُّهَا ، وَأنْتَ خَلَقْتَهَا ، وَأنتَ هَدَيْتَهَا للإسْلاَمِ ، وَأنتَ قَبَضْتَ رُوحَهَا ، وَأنْتَ أعْلَمُ بِسرِّهَا وَعَلاَنِيَتِهَا ، وَقَدْ جِئنَاكَ شُفَعَاءَ لَهُ ، فَاغْفِرْ لَهُ )) رواه أَبُو داود .

Kutoka kwake Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliomba duaa ifuatayo katika Swalaah ya jeneza: "Ee Mola, Wewe ni Rabb wake, na Wewe umemuumba, na Wewe umemuongoza katika Uislamu, na Wewe unayejua siri na dhahiri yake, nasi tumekujia waombezi wake, basi msamehe." [Abu Daawuwd]

 

 

Hadiyth – 5

وعن وَاثِلَة بنِ الأَسْقَعِ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : صَلَّى بِنَا رسول الله صلى الله عليه وسلم عَلَى رَجُلٍ مِنَ المُسْلِمِينَ ، فَسَمِعْتُهُ يَقُولُ : (( اللَّهُمَّ إنَّ فُلانَ ابْنَ فُلانٍ في ذِمَتِّكَ وَحَبْلِ جِوَارِكَ ، فَقِهِ فِتْنَةَ القَبْرِ ، وَعذَابَ النَّار ، وَأنْتَ أهْلُ الوَفَاءِ وَالحَمْدِ ؛ اللَّهُمَّ فَاغْفِرْ لَهُ وَارْحَمْهُ ، إنَّكَ أنْتَ الغَفُورُ الرَّحيمُ )) رواه أَبُو داود .

Amesema Waathilah bin Al-Asqa' (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alituswalisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), kumswalia mtu miongoni mwa Waislamu, nikamsikia akisema: "Ee Mola, hakika fulani mtoto wa fulani yupo katika dhima Yako (kwenye ahadi Yako) na kamba ya ujirani wako, hivyo muhifadhi fitna ya kaburi na adhabu ya Moto. Nawe ni Bwana wa kulipa na kuhimidiwa. Ee Mola mghufurie na umrehemu, hakika Wewe ni Mwingi wa kusamehe Mwingi wa kurehemu." [Abu Daawuwd]

 

 

 

Hadiyth – 6

وعن عبدِ الله بنِ أبي أَوْفى رضي الله عنهما : أنَّهُ كَبَّرَ عَلَى جَنَازَةِ ابْنَةٍ لَهُ أرْبَعَ تَكْبِيرَاتٍ ، فَقَامَ بَعْدَ الرَّابِعَةِ كَقَدْرِ مَا بَيْنَ التَّكْبِيرَتَيْنِ يَسْتَغْفِرُ لَهَا وَيَدْعُو ، ثُمَّ قَالَ : كَانَ رسول اللهِ صلى الله عليه وسلم يَصْنَعُ هكَذَا .

وفي رواية : كَبَّرَ أرْبَعاً فَمَكَثَ سَاعَةً حَتَّى ظَنَنْتُ أنَّهُ سَيُكَبِّرُ خَمْساً ، ثُمَّ سَلَّمَ عَنْ يَمينِهِ وَعَنْ شِمَالِهِ . فَلَمَّا انْصَرَفَ قُلْنَا لَهُ : مَا هَذَا ؟ فَقَالَ : إنِّي لاَ أزيدُكُمْ عَلَى مَا رأيْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَصْنَعُ ، أَوْ : هكَذَا صَنَعَ رسول الله صلى الله عليه وسلم . رواه الحاكم ، وقال : (( حديث صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwake 'Abdillah bin Abu Awfaa (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba alileta takbiri nne katika Swalaah ya jeneza ya binti yake. Baada ya takbiri ya nne alisimama kwa kitambo kirefu muda uliokuwa sawa na takbiri mbili huku akimuombea msamaha (maiti). Kisha akasema: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya kama nilivyofanya."

Katika riwaya nyengine: "Alipiga ya nne akakaa kidogo hadi nikadhani kuwa atapiga ya tano, kisha akatoa salamu kulia kwake. Alipoondoka tulimwambia: "Nini hiki?" akasema: "Mimi sikuzidishieni juu ya nilivyomuona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akifanya, Au: Kama hivi amefanya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). [Al Haakim na akasema Hadiyth Swahiyh]

 

 

 

Share