Skip to main content

08-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبة - Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji010-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Kilichochinjwa Kwa Ajili Ya Asiye Allaah

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

Alhidaaya.com

Vyakula Vilivyoharamishwa Na Kitabu Cha Allaah

Kilichochinjwa Kwa Ajili Ya Asiye Allaah

5-  Kilichochinjwa Kwa Ajili Ya Asiye Allaah 

Ni kama sanamu, au kiumbe, au kaburi, au maiti kama vile Sayyid Badawiy (Misri) au vinginevyo katika “matwaaghuwtw” (kila kiabudiachwo badala ya Allaah kama watu waliojivika uungu, mashaytwaan na kadhalika).

Na hii ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:

"وَمَا ذُبِحَ عَلَى النُّصُبِ"

“Na waliochinjwa kwa ajili ya ‘ibaadah ya waabudiwa”.  [Al-Maaidah: 03].