01-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila ya Elimu

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب فضل العلم تعلماً وتعليماً لله

01-Mlango Wa Fadhila ya Elimu

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

وَقُل رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا ﴿١١٤﴾

Na sema: Rabb wangu! Nizidishie Ilimu. [Twaahaa: 114]

قُلْ هَلْ يَسْتَوِي الَّذِينَ يَعْلَمُونَ وَالَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ۗ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٩﴾

Sema: Je, wanalingana sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Hakika wanakumbuka wenye akili tu. [Az-Zumar: 9]

يَرْفَعِ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ ۚ ﴿١١﴾

Allaah Atawainua wale walioamini miongoni mwenu, na waliopewa ilimu wana daraja nyingi. [Al-Mujaadalah: 11]

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ ۗ  ﴿٢٨﴾

Hakika wanaomkhofu Allaah katika Waja Wake ni ‘Ulamaa. [Faatwir: 28]

 

Hadiyth – 1

وعن معاوية رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ يُرِدِ اللهُ بِهِ خَيْراً يُفَقِّهْهُ في الدِّينِ )) . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Mu'aawiyah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kutakiwa kheri na Allaah, anamfahamisha Dini." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن ابن مسعود رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لا حَسَدَ إِلاَّ في اثْنَتَيْنِ : رَجُلٌ آتَاهُ اللهُ مَالاً ، فَسَلَّطَهُ عَلَى هَلَكَتِهِ فِي الحَقِّ ، وَرَجُلٌ آتَاهُ اللهُ الحِكْمَةَ ، فَهُوَ يَقْضِي بِهَا وَيُعَلِّمُهَا )) . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hapana kuonekana wivu ila kwa mambo mawili: Mtu aliyepewa mali na Allaah na akawa anaitumia katika njia ya haki (kujikurubisha na Allaah pamoja na kutii) na mtu ambaye amepatiwa hekima na Allaah elimu, naye anahukumia nayowatu na kuifundisha." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي موسى رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( مَثَلُ مَا بَعَثَنِي الله بِهِ مِنَ الهُدَى وَالعِلْمِ كَمَثَلِ غَيْثٍ أصَابَ أرْضاً ؛ فَكَانَتْ مِنْهَا طَائِفَةٌ طَيِّبةٌ قَبِلَتِ المَاءَ فَأَنْبَتَتِ الكَلأَ ، وَالعُشْبَ الكَثِيرَ ، وَكَانَ مِنْهَا أجَادِبُ أمْسَكَتِ المَاءَ ، فَنَفَعَ اللهُ بِهَا النَّاسَ ، فَشَرِبُوا مِنْهَا وَسَقَوْا وَزَرَعُوا، وَأَصَابَ طَائِفَةً مِنْهَا أُخْرَى إنَّمَا هِيَ قِيعَانٌ ؛ لا تُمْسِكُ مَاءً وَلاَ تُنْبِتُ كلأً ، فَذلِكَ مَثَلُ مَنْ فَقُهَ في دِينِ اللهِ ، وَنَفَعَهُ مَا بَعَثَنِي اللهُ بِهِ ، فَعَلِمَ وَعَلَّمَ ، وَمَثَلُ مَنْ لَمْ يَرْفَعْ بِذلِكَ رَأسَاً ، وَلَمْ يَقْبَلْ هُدَى اللهِ الَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ )) . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika mfano wa yale aliyonituma nayo Allaah kwa uwongofu na ilimu ni kama mfano wa mvua iliyonyesha juu ya ardhi, sehemu moja ilikuwa nzuri na yenye rutuba, nayo ikakubali hayo maji na kukamea manyasi na mimea mingi. Na sehemu nyengine ilikuwa kavu, hivyo kuyahifadhi hayo maji na Allaah kuwanufaisha watu kwa hayo maji wakanywa na kutosheka nayo na kuyatumia kwa kunnyunyizia ardhi. Mvua hii ikafika kwenye kipande cha ardhi nyingine ambayo ni jangwa (haina mimea wala miti) isiyoweza kubeba maji wala haimei nyasi. Hivyo hivyo, huo ni mfano wa walewenye kuelewa Dini ya Allaah na wakawa ni wenye kunufaika kwa yale niliyotumilizwa na Allaah, wakajifunza na kufundisha. Na mfano mwingine ni wa wale watu wasionyanyua vichwa vyao na wala hawakubali uwongofu wa Allaah uliotumwa kwao kupitia kwangu." [Al-Bukhaariy na Muslim] 

 

Hadiyth – 4

وعن سهل بن سعد رضي اللهُ عنه : أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ لِعَلِيٍّ رضي اللهُ عنه : (( فَوَاللهِ لأَنْ يَهْدِيَ اللهُ بِكَ رَجُلاً وَاحِداً خَيْرٌ لَكَ مِنْ أنْ يَكُونَ لَكَ حُمْرُ النَّعَمِ )) . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Sahl bin Sa'ad (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu): "Naapa kwa Allaah! Allaah kumuongoa mtu mmoja kupitia kwako ni bora hata kuliko ngamia wekundu." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]

 

Hadiyth – 5

وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( بَلِّغُوا عَنِّي وَلَوْ آيَةً ، وَحَدِّثُوا عَنْ بَنِي إسْرَائِيلَ وَلاَ حَرَجَ ، وَمَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّداً فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنَ النَّارِ )) . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nifikishieni japo kwa ayah moja na hadithieni mambo ya Bani Israaiyl na hapana kosa. Na nayeniongopea kwa makusudi basi ajiandalie makazi yake motoni." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 6

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( وَمَنْ سَلَكَ طَرِيقاً يَلْتَمِسُ فِيهِ عِلْماً ، سَهَّلَ اللهُ لَهُ طَرِيقاً إِلَى الجَنَّةِ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Na anayefuata njia kwa ajili ya kutafuta elimu, Allaah humsahilishia yeye njia ya kuelekea Peponi." [Muslim]

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَنْ دَعَا إِلَى هُدىً كَانَ لَهُ مِنَ الأَجْرِ مِثْلُ أُجُورِ مَنْ تَبِعَهُ لاَ يَنْقُصُ ذَلِكَ مِنْ أُجُورِهِمْ شَيْئاً )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuita watu katika uongofu atakuwa na ujira mfano wa thawabu ya wenye kumfuata wala hilo halitawapunguzia chochote katika thawabu zao." [Muslim]

 

Hadiyth – 8

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا مَاتَ ابْنُ آدَمَ انْقَطَعَ عَمَلُهُ إِلاَّ مِنْ ثَلاثٍ : صَدَقَةٍ جَارِيَةٍ ، أَوْ عِلْمٍ يُنْتَفَعُ بِهِ ، أَوْ وَلَدٍ صَالِحٍ يَدْعُو لَهُ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapofariki mwana-Aadam amali zake hukatika isipokuwa mambo matatu: Swadaqah yenye kuendelea, au elimu yenye manufaa, au mtoto mwema anayemuombea duaa." [Muslim]

 

Hadiyth – 9

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول : (( الدُّنْيَا مَلْعُونَةٌ ، مَلْعُونٌ مَا فِيهَا ، إِلاَّ ذِكْرَ الله تَعَالَى ، وَمَا وَالاهُ ، وَعَالِماً ، أَوْ مُتَعَلِّماً )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaah 'anhu) kwamba amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Jueni ya kwamba hii dunia imelaaniwa, na vimelaaniwa vilivyo ndani yake isipokuwa utajo wa Allaah Ta'aalaa na vile Anavyovipenda na mwanazuoni na mwanafunzi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 10

وعن أنسٍ رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ خَرَجَ في طَلَبِ العِلْمِ فَهُوَ في سَبيلِ اللهِ حَتَّى يَرْجِعَ )). رواه الترمذي ، وقال: (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kutoka kwa ajili ya kutafuta elimu yuko katika njia ya Allaah mpaka arudi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 11

وعن أَبي سعيدٍ الخدري رضي اللهُ عنه ، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لَنْ يَشْبَعَ مُؤْمِنٌ مِنْ خَيْرٍ حَتَّى يَكُونَ مُنْتَهَاهُ الجَنَّةَ )). رواه الترمذي، وقال: (( حديث حسن )).

Imepokewa kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Muumini hashibi kheri mpaka mwisho wake uwe ni Pepo." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 12

وعن أَبي أُمَامَة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( فَضْلُ العَالِمِ عَلَى العَابِدِ كَفَضْلِي عَلَى أدْنَاكُمْ )) ثُمَّ قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ اللهَ وَمَلاَئِكَتَهُ وَأهْلَ السَّماوَاتِ وَالأَرْضِ حَتَّى النَّمْلَةَ في جُحْرِهَا وَحَتَّى الحُوتَ لَيُصَلُّونَ عَلَى مُعَلِّمِي النَّاسِ الخَيْرَ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Abi Umamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ubora wa mwanachuoni juu ya 'Aabid (mtawa/mfanyaji 'Ibadah) ni kama ubora wangu juu ya yule aliyechini kabisa miongoni mwenu (yaani Muislamu wa kawaida)." Kisha akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Hakika Allaah, na Malaaikah Zake na viumbe wa mbinguni na ardhini na mpaka chungu katika shimo lake na nyangumi (samaki) humuombea mwenye kuwafundisha watu kheri (elimu)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 13

وعن أَبي الدرداء رضي اللهُ عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول :(( مَنْ سَلَكَ طَرِيقاً يَبْتَغِي فِيهِ عِلْماً سَهَّلَ اللهُ لَهُ طَريقاً إِلَى الجَنَّةِ، وَإنَّ المَلاَئِكَةَ لَتَضَعُ أجْنِحَتَهَا لِطَالِبِ العِلْمِ رِضاً بِمَا يَصْنَعُ ، وَإنَّ العَالِمَ لَيَسْتَغْفِرُ لَهُ مَنْ فِي السَّماوَاتِ وَمَنْ فِي الأرْضِ حَتَّى الحيتَانُ في المَاءِ ، وَفضْلُ العَالِمِ عَلَى العَابِدِ كَفَضْلِ القَمَرِ عَلَى سَائِرِ الكَوَاكِبِ ، وَإنَّ العُلَمَاءَ وَرَثَةُ الأنْبِيَاءِ ، وَإنَّ الأنْبِيَاءَ لَمْ يَوَرِّثُوا دِينَاراً وَلاَ دِرْهَماً وَإنَّمَا وَرَّثُوا العِلْمَ ، فَمَنْ أَخَذَهُ أَخَذَ بحَظٍّ وَافِرٍ )) . رواه أَبُو داود والترمذي .

Amesema Abu Dardaa' (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mwenye kufuata njia ya kutafuta elimu, Allaah humsahilishia njia yake kwenda Peponi. Na hakika Malaaikah hutandaza mabawa yao kwa mwanafunzi kwa kuridhia anayofanya. Na hakika wanazuoni huombewa msamaha na watu wa mbinguni na wale walio aidhini na mpaka na nyangumi majini. Na ubora wa mwanachuoni juu ya 'Aabiid ni kama ubora wa mwezi juu ya sayari zote nyengine. Na hakika wanazuoni ni warithi wa Manabiy. Na hakika Manabiy hawarithi dinari wala dirhamu, na bila shaka wao hurithiwa elimu. Yeyote mwenye kuchukua, hupata hisa yake kikamilifu." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]

 

Hadiyth – 14

وعن ابن مسعودٍ رضي اللهُ عنه قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( نَضَّرَ اللهُ امْرَأً سَمِعَ مِنَّا شَيْئاً ، فَبَلَّغَهُ كَمَا سَمِعَهُ ، فَرُبَّ مُبَلَّغٍ أوْعَى مِنْ سَامِعٍ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Amesema Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Allaah atamng'arisha mtu aliyesikia kutoka kwetu kitu, naye akakifikisha kama alivyokisikia. Huenda mwenye kufikishwa kutoka kwa wengine akawa ni wenye kuzingatia zuri zaidi kuliko aliyesikia mwanzo." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Hadiyth – 15

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ سُئِلَ عن عِلْمٍ فَكَتَمَهُ ، أُلْجِمَ يَوْمَ القِيَامَةِ بِلِجَامٍ مِنْ نَارٍ )) . رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال :
(( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kuulizwa kuhusu jambo (elimu) akaficha, mtu huyo atachomwa Siku ya Qiyaamah na chuma cha moto." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

Hadiyth – 16

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ تَعَلَّمَ عِلْماً مِمَّا يُبْتَغَى بِهِ وَجْهُ اللهِ عزوجل لا يَتَعَلَّمُهُ إِلاَّ لِيُصِيبَ بِهِ عَرَضاً مِنَ الدُّنْيَا ، لَمْ يَجِدْ عَرْفَ الجَنَّةِ يَوْمَ القِيَامَةِ )) يَعْنِي : رِيحَهَا . رواه أَبُو داود بإسناد صحيح .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kujifunza elimu, ambayo huwa ni kipata radhi kwa Allaah Ta'aalaa, hajifunzi isipokuwa apate mapato ya kidunia hatapata harufu ya Pepo Siku ya Qiyaamah." [Abu Daawuwd kwa Isnaad iliyo Swahiyh]

 

Hadiyth – 17

وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقول: (( إنَّ اللهَ لاَ يَقْبِضُ العِلْمَ انْتِزَاعاً يَنْتَزعهُ مِنَ النَّاسِ،وَلكِنْ يَقْبِضُ العِلْمَ بِقَبْضِ العُلَمَاءِ ، حَتَّى إِذَا لَمْ يُبْقِ عَالِماً ، اتَّخَذَ النَّاسُ رُؤُوساً جُهَّالاً ، فَسُئِلُوا فَأفْتوا بِغَيْرِ عِلْمٍ ، فَضَلُّوا وَأضَلُّوا )) . متفقٌ عَلَيْهِ .

Amesema 'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Nimemsikia Rasuli wa Alla (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakika Allaahhaichukui elimu kwa kuing'oa (toak katika nyoyo) za watu. Lakini anaichukua elimu kwa kuwafisha wanazuoni. Mpaka kutafika wakati hakutabakia mwanachuoni hata mmoja. Watu watawaweka viongozi wajinga ambao watakuwa wanaulizwa (maswali ya dini), na watatoa majibu bila ya ujuzi, watapotea (wao wenyewe) na wanapoteza (watu wengine)." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]

 

Share