06-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Anachosema Wakati wa Kulala

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب مَا يقوله عِنْدَ النوم

06-Mlango Wa Anachosema Wakati wa Kulala

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾ 

Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko ya mfuatano wa usiku na mchana, bila shaka ni Aayaat (ishara, zingatio) kwa wenye akili.

الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَـٰذَا بَاطِلًا سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴿١٩١﴾ 

Ambao wanamdhukuru Allaah wakiwa wima, au wamekaa au wamejinyoosha, na wanatafakari katika kuumbwa mbingu na ardhi (wakisema): Rabb wetu, Hukuumba haya bure, Utakasifu Ni Wako, basi Tukinge na adhabu ya moto. [Aal-'Imraan: 190-191]

 

 

Hadiyth – 1

وعن حُذَيْفَةَ ، وأبي ذرٍّ رضي الله عنهما : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا أَوَى إِلَى فِراشِهِ ، قَالَ : (( بِاسْمِكَ اللَّهُمَّ أَحْيَا وأَمُوتُ )) . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Hudhayfah na Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapojilaza kwenye godoro husema: "Bismika Allaahumma ahyaa wa amuwtu (Kwa Jina Lako, ee Rabb Wangu! Ninabaki hai na kufa)." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 2

وعن عليٍّ رضي الله عنه : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم قَالَ لَهُ ولِفَاطِمَةَ رضي الله عنهما : (( إِذَا أَوَيْتُمَا إِلَى فِرَاشِكُمَا – أَوْ إِذَا أَخَذْتُمَا مَضَاجِعَكُمَا – فَكَبِّرا ثَلاَثاً وَثَلاثِينَ ، وَسَبِّحَا ثَلاثاً وَثَلاثِينَ ، واحْمِدا ثَلاثاً وَثَلاثِينَ )) وفي روايةٍ : التَّسْبيحُ أرْبعاً وثلاثينَ ، وفي روايةٍ : التَّكْبِيرُ أرْبعاً وَثَلاَثينَ . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia yeye na Faatwimah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): "Pindi mnapoelekea kwenye kitanda au mnapolala leteni Takbira mara thelathini na tatu, na Tasbihi mara thelathini na tatu na Tahmidi mara thelathini na tatu." 

Na katika riwaayah nyingine: "Leteni Tasbihi mara thelathini na nne." 

Na katika riwaayah nyingine: "Leteni Takbira mara thelathini na nne." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا أَوَى أَحَدُكُمْ إِلَى فِرَاشِهِ فَليَنْفُضْ فِرَاشَهُ بِدَاخِلَةِ إزَارِهِ فإنَّهُ لا يَدْرِي مَا خَلَفَهُ عَلَيْهِ ، ثُمَّ يَقُولُ : بِاسمِكَ رَبِّي وَضَعْتُ جَنْبي ، وَبِكَ أرْفَعُهُ ، إنْ أَمْسَكْتَ نَفْسِي فَارْحَمْهَا ، وَإنْ أَرْسَلْتَهَا ، فاحْفَظْهَا بِمَا تَحْفَظُ بِهِ عِبَادَكَ الصَّالِحِينَ )) متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapotaka kulala mmoja wenu kwenye godoro lake kwanza akung'ute godoro lake upande wa ndani wa kikoi chake kwa kuwa haelewi alicho kiacha juu yake. Kisha aseme: 'Bismika Rabbiy wadha'tu jambi wabika arfa'uhu in amsakta nafsi farhamhaa wa in arsaltahaa fahfadhhaa bimaa Tahfadhu bihi 'Ibaadikasw Swaalihiyn (Kwa jina Lako, Rabb Wangu! Nimeuweka ubavu wangu, na kwa ajili Yako nina uinua. Kama Utaishika nafsi yangu, basi ihurumie na kama Ukiiachia Ihifadhi kwa kile Unachowahifadhia watu wema)." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]

 

Hadiyth – 4

وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها : أنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم ، كَانَ إِذَا أخَذَ مَضْجَعَهُ نَفَثَ في يَدَيْهِ ، وَقَرَأَ بالمُعَوِّذَاتِ ، ومَسَحَ بِهِمَا جَسَدَهُ . متفق عَلَيْهِ .

وفي رواية لهما : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إذا أَوَى إِلَى فِرَاشِهِ كُلَّ لَيْلَةٍ جَمَعَ كَفَّيْهِ ، ثُمَّ نَفَثَ فِيهِمَا فَقَرأَ فيهِما : (( قُلْ هُوَ اللهُ أحَدٌ ، وَقَلْ أعُوذُ بِرَبِّ الفَلَقِ ، وَقُلْ أعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ )) ثُمَّ مَسَحَ بِهِما مَا استْطَاعَ مِنْ جَسَدِهِ ، يَبْدَأُ بهما عَلَى رَأسِهِ وَوجْهِهِ ، وَمَا أقْبَلَ مِنْ جَسَدِهِ ، يَفْعَلُ ذَلِكَ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ . متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapolala hupuliza mikononi mwake Mu'awidhatain na kusoma (Al-Falaq - An- Naas) na kupaka mwili wake kwa hizo." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]

Na katka riwaayah yao nyingine: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapotaka kulala godoroni kila usiku akivishikanisha vitanga vyake, kisha akipuliza ndani yake na kusoma قُلْ هُوَ اللهُ أحَدٌ ، وَقَلْ أعُوذُ بِرَبِّ الفَلَقِ ، وَقُلْ أعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ) na kupaka mwilini mwake kwa sehemu anayoweza akianza kichwani mwake na uso wake na kuendelea kwenye sehemu yake ya mbele. Alikuwa akifanya hivyo mara tatu." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 5

وعن البراءِ بنِ عازبٍ رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا أَتَيتَ مَضْجعَكَ فَتَوَضَّأْ وَضُوءكَ لِلصَّلاَةِ ، ثُمَّ اضْطَجِعْ عَلَى شِقِّكَ الأيْمَن ، وَقُلْ : اللَّهُمَّ أَسْلَمْتُ نَفْسِي إِلَيْكَ، وَوَجَّهْتُ وَجْهِي إِلَيْكَ، وَفَوضْتُ أَمْرِي إليكَ ، وأَلْجَأتُ ظَهرِي إلَيْكَ ، رَغْبَةً وَرهْبَةً إليكَ ، لا مَلْجَأَ وَلاَ مَنْجَا مِنْكَ إِلاَّ إليكَ ، آمَنْتُ بِكِتابِكَ الَّذِي أنْزَلْتَ، وَبِنَبِيِّكَ الَّذِي أرْسَلْتَ، فإنْ مِتَّ مِتَّ عَلَى الفِطْرَةِ ، وَاجْعَلْهُنَّ آخِرَ مَا تَقُولُ )) متفق عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Al-Baraa' bin 'Azib (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliniambia: "Unapoenda kulala (kwanza) tawadha wudhu wako wa Swalaah, kisha lala kwa ubavu wa kuliyani, kisha sema: Allaahumma inniy aslamtu wajhi Ilayka. Wa Fawwadhtu amriy Ilayka wa alja'tu dhahriy Ilayka raghbatan wa rahbatan Ilayka. Laa maljaa walaa manjaa Minka illaa Ilayka. Aamantu Bikitaabikal ladhiy anzalta wa Binabiyyikal ladhiy arsalta (Ee Rabb Wangu! Hakika nimeukabidhi uso wangu Kwako. Na jambo langu nimeliegemeza Kwako. Na mgongo wangu nimeugeuza Kwako. Hali ya kupenda na kuhofu Kwako. Hakuna pa kukimbilia wala pa kusalimika na Wewe isipokuwa Kwako. Nimekiamini Kitabu Chako ambacho Umekiteremsha, na Nabiy Wako ambaye Umemtuma). Kama utakufa usiku wako huo, basi utakufa katika fitra (Uislamu). Na hayo uyafanye ndiyo mwisho wa maneno yako." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]

 

 

Hadiyth – 6

وعن أنس رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا أَوَى إِلَى فِرَاشِهِ قَالَ : (( الحَمْدُ للهِ الَّذِي أَطْعَمَنَا وَسَقَانَا ، وكفَانَا وآوانَا ، فَكَمْ مِمَّنْ لا كَافِيَ لَهُ وَلاَ مُؤْوِيَ )) . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapolala godoroni mwake, akisema: "AlhamdulliLLaahi Ladhiy atw'amanaa wa saqaanaa wa kafaanaa wa aaawaanaa fakam mimman laa kaafiya lahu walaa mu'wiya (Sifa zote njema anastahiki Allaah ambaye Ametulisha na Kutunywesha na Kututosheleza na kutupatia hifadhi (makazi), kwani wapo wangapi wasiokuwa na vya kuwatosheleza wala makao)." [Muslim]

 

Hadiyth – 7

وعن حذيفة رضي الله عنه : أنَّ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا أَرَادَ أَنْ يَرْقُدَ ، وَضَعَ يَدَهُ اليُمْنَى تَحْتَ خَدِّهِ، ثُمَّ يَقُولُ : (( اللَّهُمَّ قِني عَذَابَكَ يَوْمَ تَبْعَثُ عِبَادَكَ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

ورواه أَبُو داود ؛ من رواية حَفْصَةَ رَضِيَ اللهُ عنها ، وفيهِ أنه كَانَ يقوله ثلاث مراتٍ .

Imepokewa kutoka kwa Hudhayfah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapotaka kulala huweka mkono wake wa kuume chini ya shavu lake, kisha akisema: "Allaahumma Qiniy 'Adhaabaka yawma tab'athu 'Ibaadaka (Ee Rabb Wangu! niepushe na adhabu Yako siku Utakayo wafufua waja Wako)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

Na imepokewa na Abu Daawuwd kutoka kwa Hafswah (Radhwiya Allaahu 'anhaa), amesema: "Alikuwa akirudia mara tatu."

 

 

Share