Faharasa: Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake: Tarjama Ya Alhidaaya.com

 

Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake   

 

Maana Zake Kwa Mukhtasari

 

Alhidaaya.com

 

 

Jina/

Swiffah

 

Tamshi

Maana

 

الرّب

 

Ar-Rabb

 

Rabb Wa Kila Kitu, Mola, Bwana, Muumbaji, Msimamizi, Mneemeshaji, Mfalme, Mwenye Kuruzuku, Mwendeshaji wa Mambo, Mlezi.

 

 

الله

Allaah

 

Mwenye Uluwhiyyah, Mwenye ‘Ubuwdiyyah

 

 

الملك

Al-Malik

 

Mfalme

 

 

المالك

Al-Maalik

 

Mwenye Kumiliki

 

 

الّذي له الملك

Alladhiy

Lahul-Mulk

 

Ambaye Ufalme ni Wake

 

الواحد

Al-Waahid

 

Mmoja Pekee Asiye Na Mfano

 

 

الأحد

Al-Ahad

 

Mpweke Asiye Na Mshirika

 

الصّمد

Asw-Swamad

 

Mwenye Kukusudiwa Kwa Haja Zote

 

العليم

Al-‘Aliym

 

 

Mjuzi Wa Yote Daima

الخبير

Al-Khabiyr

 

Mjuzi Wa Undani Na Kina Cha Mambo, Mwenye Ujuzi Wa Ya Dhahiri Na Ya Siri

 

الحكيم

Al-Hakiym

 

Mwenye Hikmah Wa Yote Daima

 

الرّحمن

Ar-Rahmaan

 

Mwingi Wa Rehma

 

 

الرّحيم

Ar-Rahiym

Mwenye Kurehemu 

 

 

البرّ

Al-Barr

 

Mwingi Wa Ihsani

 

 

الكريم

Al-Kariym

 

Karimu, Mtukufu

 

 

الجوّاد

Al-Jawwaad:

 

Mwingi wa Ukarimu

 

 

الرّؤف

Ar-Rauwf

 

Mwenye Huruma Mno

 

 

الواهَاب

Al-Wahhaab

 

Mwingi Wa Kutunuku, Mpaji Wa Yote

 

السّميع

As-Samiy’i

 

Mwenye Kusikia Yote Daima

 

 

البصير

Al-Baswiyr

 

Mwenye Kuona Yote Daima

 

 

الحميد

Al-Hamiyd

 

Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa

 

 

المجيد

Al-Majiyd

 

Mwingi Mno Wa Vipawa Na Ukarimu

 

 

الكبير

Al-Kabiyr

 

Mkubwa Wa Dhati, Vitendo Na Sifa

 

 

العظيم

Al-‘Adhwiym

 

Adhimu, Mwenye Taadhima

 

 

الجليل

Al-Jaliyl

 

Jalali, Mwenye Ujalali, Mtukuka Daima, Mwenye Hadhi

 

العفوّ

Al-‘Afuww

Mwingi Wa Kusamehe

 

 

الغفور

Al-Ghafuwr

 

Mwingi Wa Kughufiria, Kusitiri

 

 

الغفّار

Al-Ghaffaar

 

Mwingi Wa Kughufuria, Kusitiri Mara Kwa Mara

 

التواب

At-Tawwaab

 

Mwingi Wa Kupokea Toba Baada Ya Toba

 

 

القدّوس

Al-Qudduws

 

Mtakatifu, Ametakasika Na Sifa Zote Hasi

 

السّلام

As-Salaam

 

Mwenye Amani, Mwenye Kusalimika Na Kasoro Zote

 

الْعَلِيُّ

Al-‘Aliyy

 

Ametukuka, Ana Uadhama Kuliko wote, kuliko vyote, Yuko juu Kabisa juu ya Viumbe Vyake vyote.

 

الأعلى

Al-A’laa

 

Mwenye Uluwa Na Taadhima Kuliko Vyote

 

العزيز

Al-‘Aziyz

 

Mwenye Nguvu, Mshindi Asiyeshindika Daima

 

القوي

Al-Qawiyy

 

Mwenye Nguvu

المتين

Al-Matiyn

 

Mwenye Nguvu Na Shadidi, Madhubuti

 

الجبّار

Al-Jabbaar

 

Jabari, Mwenye Kulazimisha, Mwenye Kuunga

 

المتكبّر

Al-Mutakabbir

 

Mwenye Kustahiki Kutakabari, Yuko Juu Ya Viumbe

 

الخالق

Al-Khaaliq

 

Muumbaji

البارء

Al-Baariu

Muumbaji Wa Viumbe Kwa Maumbile Yanayonasibiana Na Mazingira Ya Maisha Yao

 

المصوّر

Al-Muswawwir

 

Muundaji Sura Na Umbo

 

المؤمن

Al-Muumin

 

Mwenye Kusadikisha Ahadi, Mwenye Kuaminisha

 

المهيمن

Al-Muhaymin

 

Mwenye Kutawalia Na Kuendesha

 

القدير

Al-Qadiyr

 

Muweza Wa Yote Daima

اللّطيف

Al-Latwiyf

 

Latifu, Mwenye Kudabiri Mambo Kwa Utuvu, Mjuzi Wa Ya Dhihiri Na Ya Siri

 

الحسيب

Al-Hasiyb

 

Mwenye Kuhesabu, Kutosheleza

 

الرقيب

Ar-Raqiyb

 

Mwenye Kuchunga

الحفيظ

Al-Hafiydhw

 

Mwenye Kuhifadhi, Kulinda

 

المحيط

Al-Muhiytw

Mwenye Kuzunguka Vyote

 

القهّار

Al-Qahhaar

 

Mwenye Kuteza Nguvu Asiyepingika

 

القاهر

Al-Qaahir

 

Mwenye Kuteza Nguvu, Asiyepingika

 

المقيت

Al-Muqiyt

 

Mwenye Kuruzuku Chakula

 

الوكيل

Al-Wakiyl

 

Mtegemewa Kwa Yote, Msimamizi

 

ذو الجلال والإكرام

Dhul-Jalal

Wal-Ikraam

 

Mwenye Ujalali Na Ukarimu, Mtukuka daima, Mwenye Utukufu wa Juu Kabisa, Taadhima, Hadhi.  

 

الودود

Al-Waduwd

 

Mwenye Mapenzi Tele Halisi

الفتّاح

Al-Fattaah

 

Mwingi Wa Kufungua, Kuhukumu

 

الرّزاق

Ar-Razzaaq

 

Mwingi Wa Kuwaruzuku Viumbe Vyote

 

الحكم

Al-Hakam

 

Hakimu Mwadilifu Wa Haki Zaidi Kuliko Wote

 

العدل

Al-‘Adl

 

Mwadilifu Kuliko Wote

جامع الناس

Jaami’un-Naas

 

Mwenye Kuwakusanya Watu

 

الحيّ

Al-Hayyu

 

Aliye Hai Daima

القيّوم

Al-Qayyuwm

 

Msimamizi Wa Kila Jambo Milele

 

النور

An-Nuwr

 

Mwenye Nuru, Mwanga

بديع السماوات والأرض

Badiy’us-Samaawaat

Wal-Ardhw

Mwanzishaji wa Mbingu na Ardhi

 

القابض

Al-Qaabidhw

 

Mwenye Kuchukua

الباسط

Al-Baasitw

 

Mwenye Kukunjua

المعطي

Al-Mu’twiy

 

Mpaji

المانع

Al-Maani’u

 

Mwenye Kuzuia

الشهيد

Ash-Shahiyd

Shahidi Mwenye Kujua Vyema Yenye Kuonekana Na Yasiyoonekana, Mwenye Kushuhudia

 

المبدء

Al-Mubdiu

 

Mwanzishaji

المعيد

Al-Mu’iyd

 

Mrejeshaji

الفعّال لما يريد

Al-Fa-‘aalu Limaa Yuriyd

 

Mwenye kufanya Atakacho

الغني

Al-Ghaniyy

 

Mkwasi Amejitosheleza, Hahitaji Lolote

 

المغني

Al-Mughniy

 

Al-Mughniy

 Mkwasi,

Amejitajirisha

 

الحليم

Al-Haliym

 

Mpole Wa Kuwavumilia Waja

الشّاكر

Ash-Shaakir

 

Mwenye Kupokea Shukurani

الشكور

Ash-Shakuwr

 

Mwingi Wa Shukrani, Mwingi Wa Kukubali Kidogo Kwa Thawabu Tele

 

القريب

Al-Qariyb

 

Aliye Karibu

المجيب

Al-Mujiyb

 

Mwenye Kuitikia

 

الكافي

Al-Kaafiy

 

Aliyejitosheleza

الأوّل

Al-Awwal

 

Wa Kwanza Bila Mwanzo

الآخر

Al-Aakhir

 

Wa Mwisho, Hapana Kitu Baada Yake

 

الظّاهر

Adhw-Dhwaahir

 

Dhahiri Kwa Vitendo Vyake

الباطن

Al-Baatwin

 

Asiyeonekana Na Viumbe

الواسع

Al-Waasi’u

 

Aliyeenea

الهادي

Al-Haadiy

 

Mwenye Kuongoza

الرّشيد

Ar-Rashiyd

 

Mwenye Kuelekeza, Kuongoza

الحق

Al-Haqq

Wa Haki, Wa Kweli

 

العالم

Al-‘Aalim

 

Mjuzi wa Yote Daima

الحفي

Al-Hafiyy

 

Mwenye Kutoa Utukufu

الأكرم

Al-Akram

 

Mkarimu Kuliko Wote

الإله

Al-Ilaah

 

Ilaah - Mwabudiwa Wa Haki

الخلاّق

Al-Khallaaq

 

Muumbaji Wa Kila Namna Kwa Wingi 

 

المليك

Al-Maliyk

 

Mfalme Mwenye Nguvu Daima

 

المبين

Al-Mubiyn

 

Mwenye Kubainisha

المولى

Al-Mawlaa

 

Maula, Rafiki Mwandani Wa Karibu, Mlinzi, Msaidizi, Msimamizi, Bwana Mlezi.

  

المقتدر

Al-Muqtadir

 

Mwenye Uwezo Wa Juu Kabisa

 

المتعّال

Al-Muta’aal

 

Mwenye Uluwa Na Taadhima

القادر

Al-Qaadir

 

Mwenye Uwezo

الوارث

Al-Waarith

Mrithi Kwa Kuondosha Viumbe Wote Na Kubaki Yeye Tu

 

الولي

Al-Waliyyu

 

Walii, Aliye Karibu

النصير

An-Naswiyr

Mwenye Kunusuru, Msaidizi

 

 

 

Share