017-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Wanaume Kujipaka Zafarani Au Hina

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

 

اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ 

Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume 

 

Alhidaaya.com 

 

 

 

017-  Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume:  Wanaume Kujipaka Zafarani Au Hina:

 

 

·        Ni Marufuku Kujipaka Zafarani

 

Zafarani ni mmea wa kinjano ambao hutumika kwa kutia rangi nguo, na kama manukato kwa wanawake ambao hujipaka nao mwili.  Haijuzu kwa mwanaume kuutumia. 

 

Anas amesema: 

 

"نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يَتَزَعْفَرَ الرَّجُلُ"

 

“Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza mwanaume kutumia zafarani”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5846) na Muslim (1101)].

 

‘Ammaar bin Yaasir:  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalhi wa sallam) amesema:

 

"ثَلَاثٌ لَا تَقْرَبُهُمُ الْمَلَائِكَةُ :جِيفَةُ الْكَافِرِ ، وَالْمُتَضَمِّخُ بِالْخَلُوقِ ، وَالْجُنُبُ إِلَّا أَنْ يتَوَضَّأ"

 

“Watu watatu hawakurubiwi na Malaika:  Mzoga wa kafiri, mwenye kujipaka “khaluwq”, na mwenye janaba mpaka atawadhe”.  [Hadiyth Hasan Lighayrihi.  Imekharijiwa na Abu Daawuwd, iko kwenye Swahiyh Al-Jaami’i (3061)].

 

“Khaluwq” ni manukato ya kinjano yaliyotengenezwa kutokana na zafarani, hutumiwa na wanawake tu.

 

·        Je, Mwanaume Anaruhusiwa Kujipaka Mikono Na Miguu Yake Hina Na Mfano Wake?

 

Abu Hurayrah: 

 

"أُتِيَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِمُخَنَّثٍ قَدْ خَضَبَ يَدَيْهِ وَرِجْلَيْهِ بِالْحِنَّاءِ ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ‏"‏مَا بَالُ هَذَا؟‏"‏ ‏.‏ فَقِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، يَتَشَبَّهُ بِالنِّسَاءِ ‏.‏ فَأُمِرَ بِهِ فَنُفِيَ إِلَى النَّقِيعِ ، فَقَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَلاَ نَقْتُلُهُ؟ فَقَالَ: ‏"‏إِنِّي نُهِيتُ عَنْ قَتْلِ الْمُصَلِّينَ"

 

“Khanithi aliyekuwa amepaka mikono na miguu yake hina, aliletwa kwa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam).  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akauliza:  Ana nini huyu?  Akaambiwa:  Ee Rasuli wa Allaah, huyu anajifananisha na wanawake.  Rasuli akaamuru apelekwe uhamishoni Naqiy.  Wakasema:  Ee Rasuli wa Allaah!  Kwa nini tusimuue?  Akasema:  Nimekatazwa kuua wenye kuswali”.  [Al-Albaaniy kasema ni Swahiyh.  Imekharijiwa na Abu Daawuwd].

 

Al-Haafidh amesema:  “Ama kupaka mikono na  miguu, hili haliruhusiwi kwa mwanamume ila kwa matibabu tu”.   [Fat-hul Baariy (10/367].

 

Ninasema:  “Na Hadiyth zinazokataza kujipaka zafarani zinatilia nguvu hilo.  Ama Hadiyth ya Anas:

 

“Kwamba Abdurrahmaan bin ‘Awf alikuja kwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa na alama ya kinjano, Rasuli akamuuliza, naye akamweleza kwamba ameoa mwanamke wa Kianswaar”,.. Hadiyth hii haina ubavu wa kutolewa dalili juu ya kujuzu mwanaume kujipaka zafarani, na hasa pale An-Nawawiy alipoweka wazi zaidi kwa kusema:  “Unjano huo ulimganda toka kwa mkewe”.  [Sharhu Muslim]

 

Na kwa muktadha huu, wanalolifanya mabwana harusi wengi katika “Usiku Wa Hina” la kutia hina mikono na miguu kabla ya ndoa, jambo hili halijuzu.  Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.

 

 

Share