08-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Kivazi Cha Mwanamke: Sehemu Ya Nguo Ya Mwanamke Inayoburuza Chini

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

  

لِبَاسُ المَرْأَةِ

Kivazi Cha Mwanamke 

 

Alhidaaya.com 

 

 

 

008-Sehemu Ya Nguo Ya Mwanamke Inayoburuza Chini:

 

Ummu Salamah: 

 

"قُلْتُ لِرَسُولِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حِينَ ذُكِرَ الإِزَارُ: فَالْمَرْأَةُ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: ‏تُرْخِيهِ شِبْرًا، ‏‏قُلْتُ: إِذًا يَنْكَشِفُ عَنْهَا، قَالَ: ‏فَذِرَاعًا لاَ تَزِيدُ عَلَيْهِ‏"

 

“Nilimwambia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati ilipotajwa izari (ifike wapi kwa mwanaume):  Na vipi kuhusu  mwanamke ee Rasuli wa Allaah?  Akasema:  Ateremshe shubiri.  Nikasema:  Ikiwa hivyo, basi miguu (kwato) itaonekana (wakitembea).  Akasema:  Basi iwe dhiraa, na isizidi zaidi ya hapo”.  [Abu Daawuwd (4117), na Maalik katika Al-Muwattwa (1700) kwa Sanad Swahiyh].

 

Hadiyth hii inathibitisha kwamba wanawake wako nje ya duara la makamio yanayowahusu wanaume wenye kuburura nguo.  ‘Ulamaa kwa sauti moja wanasema kwamba inajuzu mwanamke kuteremsha nguo yake chini ya vifundo viwili vya miguu.    

 

Ingia kwenye tovuti upate kujua urefu halisi wa dhiraa na shubiri.

                                                                                                                                        

Faida:

 

Ni kutokea wapi inapimwa shubiri ambayo mwanamke anaiteremsha nguo yake?

 

Shubiri hupimwa toka nusu ya muundi kama ilivyonukuliwa katika Kitabu cha ‘Awnul Ma’abuwd (11/174).  Na kwa ajili hiyo, Ummu Salamah akasema kwamba kwato za miguu yao zitaonekana, na hapo Rasuli akawaruhusu kuteremsha dhiraa.  Na makusudio hapa, ni kumzindua mwanamke ajue mambo mawili.  La kwanza, ni kuwa ni wajibu kwake afunike kwato zake mbili kwa nguo yake, na pili ni kwamba inajuzu kuiteremsha nguo yake kwa kiasi cha kutozidi dhiraa kama tulivyotangulia kusema.

 

 

 

Share