05-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo: Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu: "النَّمْصُ" Ni Haramu

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ 

Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo

 

 

الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ

Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu

 

 

Alhidaaya.com

 

 

05- "النَّمْصُ"   Ni Haramu:

 

"النَّمْصُ" ina maana mbili.  Ya kwanza ni kuondosha nywele za uso wote, na ya pili ni kuondosha nyusi au kuzichonga, si uso wote.  Maana hii ya pili ndiyo iliyonukuliwa toka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa), na yeye ndiye ajuaye zaidi mfano wa jambo kama hili kuliko mwingine yeyote.

 

Kuchonga nyusi ni haramu, ni sawa kwa ajili ya mume au kwa mwingine, kwa idhini yake au bila idhini, kwa kuwa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

"لَعَنَ النَّامِصَةَ وَالْمُتَنَمِّصَةَ"

 

“Amemlaani mchonga nyusi na mwenye kuchongwa”.  [Al-Bukhaariy (5948), Muslim (2125) na wengineo]

 

Rasuli amekilaani kitendo hiki kwa kuwa ni ubadilishaji wa uumbaji wa Allaah, na hivyo kinakuwa ni haramu kwa mchongaji na mchongwa.

 

Lakini pamoja na laana hii ya Allaah na Rasuli Wake kwa wanaofanya jambo hili, tunaona -kwa masikitiko makubwa- kuwa jambo hili limeenea sana kwa wanawake wa Kiislamu na hata kwa wanaovaa hijabu kufikia mpaka wa kuonwa ajabu kwa wasiolifanya na kuchezwa shere. 

 

Mwanamke Akitokezewa na Nywele Za Sharubu Au Ndevu Basi Aziondoshe:

 

Katika baadhi ya hali ambazo si za kawaida, huota kwa baadhi ya wanawake nywele za sharubu au ndevu hadi kutisha.  Ikiwa hivyo, anatakikana aziondoshe, kwa sababu atakuwa anarejesha umbile katika asili yake na si kulibadilisha.

 

 

 

Share