12-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo: Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu: Pambo La Wanja

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ 

Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo

 

 

الزِّيْنَةُ للمَرْأَةِ المُسْلِمَةِ

Pambo Kwa Mwanamke Wa Kiislamu

 

Alhidaaya.com

 

 

12-Pambo La Wanja:

 

Inapendeza kwa mwanamke ajitie wanja ili kujipamba kwa mumewe.  Pia kwa ajili ya dawa kama atasumbuliwa na maumivu ya jicho.

 

Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"وَإِنَّ خَيْرَ أَكْحَالِكُمُ الإِثْمِدُ، يَجْلُو الْبَصَرَ، وَيُنْبِتُ الشَّعْرَ‏"

 

“Na hakika wanja wenu ulio bora zaidi ni wa “al-ithmid”, unasafisha macho, unaotesha kope”.  [Hadiyth Hasan.  Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3878), At-Tirmidhiy (994), An-Nasaaiy (8/15) na Ibn Maajah (3497)].

 

Mwanamke haruhusiwi kujitia wanja wakati wa eda ya kufiwa na mumewe.

 

Haijuzu Kutumia Kichupa Cha Wanja Cha Dhahabu Au Silva

 

Katika mlango wa vyombo, tulieleza kwamba haijuzu kutumia vyombo vya dhahabu au silva kwa kuwa kufanya hivyo ni sehemu ya israfu, kibri, kuvunja nyoyo za masikini na mfano wa hayo.

 

 

Share