028-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Qaswasw: Aayah (51): وَلَقَدْ وَصَّلْنَا لَهُمُ الْقَوْلَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

028-Asbaab Nuzuwl Al-Qaswasw Aayah 51

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَلَقَدْ وَصَّلْنَا لَهُمُ الْقَوْلَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ ﴿٥١﴾

51. Na kwa yakini Tumewafuatilishia na kuwateremshia sehemu kwa sehemu ya Neno ili wapate kukumbuka. [Al-Qaswas (28:51)]

 

  

Sababun-Nuzuwl: 

 

Ibn Jariyr katika Mujallaad wa 20 ukurasa wa 88 amesema: “Amenihadithia Bishr bin Aadam amesema, ametuhadithia ‘Affaan bin Muslim amesema, ametuhadithia Hammaad bin Salamah amesema, ametuhadithia ‘Amri bin Diynaar toka kwa Yahyaa bin Ja-’adah amesema: Aayah hii iliteremka kuwazungumzia watu kumi mimi nikiwa mmoja wao:

 

وَلَقَدْ وَصَّلْنَا لَهُمُ الْقَوْلَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ

 

Na kwa yakini Tumewafuatilishia na kuwateremshia sehemu kwa sehemu ya Neno ili wapate kukumbuka. [Al-Qaswas (28:51)]

 

[Hadiyth hii imekharijiwa na At-Twabaraaniy katika Mujallaad wa Tano kurasa za 46 na 47. Al-Haythamiy amesema katika Majma’u Az Zawaaid Mujallaad wa Saba ukurasa wa 88 kuwa imesimuliwa na At-Twabaraaniy kwa Isnaad Mbili; moja ikiwa Muttaswil na wapokezi wake ni watu wa kuaminika, nayo ni hii, na nyingine yenye Isnaad iliyokatika]

 

 

 

Share