19-Malaika: Malaika Wenye Sura Na Maumbo Ya Kutisha: (2)- Zabaaniyah Wa Jahannam

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

19:  Malaika Wenye Sura Na Maumbo Ya Kutisha

 

(2)-  Zabaaniyah Wa Jahannam

 

 

Allaah Ta’aalaa Anasema:

 

"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّـهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ"

 

Enyi walioamini!  Jikingeni nafsi zenu pamoja na ahli zenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe.  Wanaulinda Malaika washupavu wasio na huruma, wakali, hawamuasi Allaah kwa yale Anayowaamrisha na wanafanya yale wanayoamrishwa”. [At-Tahriym: 06]

 

Malaika hawa inaonyesha wako chini ya mkuu wao Maalik, kazi yao ni kuwatesa watu wa motoni, kuwadhalilisha na kuwadhibiti.

 

Ibn Kathiyr akielezea maana ya "شِدَادٌ"  amesema:  “Wameumbwa kwa maumbile yaliyo kwenye ukomo wa ukali, nguvu na mwonekano wa kukera na kutisha. Hawa ndio “Zabaaniyah”. Tunamwomba Allaah Atulinde tusikutane nao.

 

As-Sa’adiyy naye kasema akilielezea neno hilo hilo:  “Tabia zao ni ngumu mno, wanakemea kwa ukali uliopitiliza, sauti zao zinaogopesha mno, na wanaogopesha mno ukiwaona.  Watakuwa wakiwadhalilisha watu wa motoni kwa nguvu walizopewa na Allaah”.

 

 

Share