Khomeini Ndani Ya Darubini - 2: Hoja Yake Kwamba Maimaamu Wa Shia Ni Bora Kuliko Malaika Wote Na Manabii

Khomeini Ndani Ya Darubini – 2

Hoja Yake Kwamba Maimaamu Wa Shia Ni Bora

Kuliko Malaika Wote Na Manabii

 

Imeandikwa na Wajiyh Al-Madini Toleo la Pili

Alhidaaya.com

 

 

 
 

Ndani ya kitabu chake “Serikali ya Kiislamu” (The Islamic Government), Khomeini amesema “Ni ukweli, Imaam ana sehemu ya kushukuriwa, hadhi ya utukufu na mfalme wa dunia ambapo utawala na amri zinajisalimisha kwa nukta (atoms) zote za dunia. Kwa enzi za dini yetu ni kwamba Imaamu wana sehemu ya kushukuriwa ambayo haipatikani kwa Malaika wa karibu wala kwa Rasuli….Kulingana na kauli na tamaduni ambazo zipo mikononi mwetu, Rusuli na Imaamu watukufu, Rehma na Amani ziwe juu yao, walikuwa ni mwangaza kabla ya kuumbwa kwa dunia hii, kisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akawafanya wana nafasi (muhimu) kwa Allaah ambayo haijapata kuzungukwa na Malaika au Rasuli yeyote.

 

 

 

Tokea kuchapishwa kwa kitabu hiki, wanazuoni wa Kiislamu wamekuwa wakitoa maneno wazi wazi kumtuhumu Khomeini kwa Kufru na kurtadi kwa sababu zifuatazo:-

 

 

1-Hamna aya ndani ya Qur-aan wala Hadiyth Swahihi kutoka kwa Rasuli wa Allaah inayoeleza utukufu au Imaamu wa dai la Imaamu, achilia mbali zile tuhuma za hadhi zinazohusiana nao.

 

 

2-Yale maneno ya “Msaidizi Mtawala wa Ulimwengu” unaeleza, kwa mujibu wa msimaamo wa Khomeini kwamba Imaamu hao wakisema kwa kitu “kuwa”, kinakuwa (“….na kwao zinajisalimisha nukta za ulimwengu.”) Hii hakika ni sifa iliyofungika kwa Allaah tu, Muumbaji, ambaye ametakasika na udhaifu wowote. Anasimaama bila ya mshirika au msaada katika uumbaji na wala hamna wa kugawana naye mamlaka yake, kama anavyosema:

 

قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِ اللَّـهِ ۖ لَا يَمْلِكُونَ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ وَمَا لَهُمْ فِيهِمَا مِن شِرْكٍ وَمَا لَهُ مِنْهُم مِّن ظَهِيرٍ ﴿٢٢﴾

Sema: Ombeni wale mnaodai kwa dhana (ni waabudiwa) badala ya Allaah, hawamiliki hata uzito wa sisimizi mbinguni wala ardhini, na wala hawana humo ushirika Naye, na wala Yeye (Allaah) Hana msaidizi miongoni mwao. [Sabaa:22]

 

Sifa ni zake Yeye pekee, pia Anasema:

 

تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ الْمُلْكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿١﴾

Amebarikika Ambaye Mkononi Mwake umo ufalme Naye juu ya kila kitu ni Muweza. [Al-Mulk:1]

 

Mamlaka yote yapo ndani ya mikono ya Allaah pekee, harithishi chembe yoyote kwa watumwa (waja) Wake.

 

 

أَمِ اتَّخَذُوا آلِهَةً مِّنَ الْأَرْضِ هُمْ يُنشِرُونَ ﴿٢١﴾ لَوْ كَانَ فِيهِمَا آلِهَةٌ إِلَّا اللَّـهُ لَفَسَدَتَا ۚ فَسُبْحَانَ اللَّـهِ رَبِّ الْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ ﴿٢٢﴾ لَا يُسْأَلُ عَمَّا يَفْعَلُ وَهُمْ يُسْأَلُونَ ﴿٢٣﴾ أَمِ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ آلِهَةً ۖ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ ۖ هَـٰذَا ذِكْرُ مَن مَّعِيَ وَذِكْرُ مَن قَبْلِي ۗ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ الْحَقَّ ۖ فَهُم مُّعْرِضُونَ ﴿٢٤﴾ وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ ﴿٢٥﴾ وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَـٰنُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۚ بَلْ عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ ﴿٢٦﴾ لَا يَسْبِقُونَهُ بِالْقَوْلِ وَهُم بِأَمْرِهِ يَعْمَلُونَ ﴿٢٧﴾ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ارْتَضَىٰ وَهُم مِّنْ خَشْيَتِهِ مُشْفِقُونَ ﴿٢٨﴾ وَمَن يَقُلْ مِنْهُمْ إِنِّي إِلَـٰهٌ مِّن دُونِهِ فَذَٰلِكَ نَجْزِيهِ جَهَنَّمَ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ ﴿٢٩﴾

Je, wamechukua waabudiwa katika ardhi wanaofufua?  Lau wangelikuweko humo (mbinguni na ardhini) waabudiwa badala ya Allaah, bila shaka zingelifisidika. Basi Subhaana Allaah! Utakasifu ni wa Allaah Rabb wa ‘Arsh kutokana na ambayo wanavumisha.  Haulizwi (Allaah) kwa yale Anayoyafanya, lakini wao wataulizwa.. Je, wamejichukulia badala Yake waabudiwa? Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآلهوسلم): Leteni burhani yenu. Hii (Qur-aan) ni ukumbusho wa walio pamoja nami, na ni ukumbusho wa walio kabla yangu; bali wengi wao hawajui haki; kisha wao ni wenye kukengeuka. Na Hatukutuma kabla yako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Rasuli yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: Hakika hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi; basi Niabuduni. Na wakasema: Ar-Rahmaan Amejifanyia mwana! Subhaanah! Utakasifu ni Wake! Bali (hao) ni waja waliokirimiwa. Hawamtangulii (Allaah) kwa kauli, nao kwa amri Yake wanatenda. Anajua yale yaliyoko mbele yao, na yale yaliyoko nyuma yao, na wala hawataomba shafaa’ah (yeyote) isipokuwa kwa yule ambaye (Allaah) Amemridhia, nao kutokana na kumkhofu, ni wenye khofu na kutahadhari. Na yeyote yule miongoni mwao atakayesema: Mimi ni mwabudiwa badala Yake, basi huyo Tutamlipa Jahannam. Hivyo ndivyo Tunavyolipa madhalimu. [Al-Anbiyaa: 26-29]

 

 

Hivyo, malaika wote ambao ni watumwa wa karibu kwa Allaah hawana amri juu ya madaraka yao wenyewe, na hawana mgao wa utawala wa Allaah.

 

 

Vivyo hivyo, wajumbe wote wa Allaah, ambao ni binaadamu bora, hawana chochote kwenye mgao wa Allaah; Allaah Anazungumza juu ya mbora wao wote, Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam). Allaah Anasema:

 

قُل لَّا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللَّـهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ ….﴿٥٠﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Sikuambieni kuwa mimi nina hazina ya Allaah; na wala kwamba najua ya ghayb [Al-An’aam:50]

 

Maneno hayo pia yalizungumzwa na Nuuh kwa watu wake, Allaah pia Amemtambulisha Mtume Wake:

 

قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي نَفْعًا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَاءَ اللَّـهُ ۚ ﴿١٨٨﴾

Sema: Siimilikii nafsi yangu manufaa yoyote wala dhara yoyote isipokuwa Apendavyo Allaah. [Al-A’raaf: 188]

 

 

Kama ni Rasuli wa Allaah na Malaika Wake hawana nguvu ya kujifanyia nafuu au dhara, wala hawana amri juu ya shughuli zozote, isipokuwa wao wote ni watumwa walio chini ya Allaah, na wao wanalazimika kutii amri zake, yale madai kwamba Imaamu waliotuhumiwa kuwa na mamlaka juu ya nukta (atoms) za Ulimwengu na wakaitakidi kuwa wana nafasi ya Msaidizi wa Mtawala wa Ulimwengu (si chochote) ila ni kufru iliyo wazi, iso na imani na shirk, au kumfanya Allaah kuwa na washirika kwenye Uungu wake pekee, Bwana wa Ulimwengu, Mtukufu Aliyetakasika na yote wanayompa Yeye. Yale madai kwamba Imaamu wana hadhi ya kipekee kwa Allaah haijapatikana kwa Malaika wa karibu wala Mjumbe aliyeletwa ni uongo ulionasibishwa kwa hao imaamu; ni tamko la unafiki na kurtadi.

 

 

3-Tamko la kwamba Imaamu na Rusuli walikuwa ni nuru kabla ya kuletwa (duniani) ni kufru, na haijathibitishwa ndani ya Qur-aan, Sunnah au makubaliano (Shuura) ya Waislamu. Ni uongo wa kufru ambayo wanafiki kutoka taifa la Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) inafanana na ndugu zao wa taifa ambalo linaamini kuwa Yesu ni mwana wa Allaah, Rusuli wote wameumbwa (kama) binaadamu kama Allaah Anavyosema:

 

قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰ ﴿١١٠﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi ni mtu kama nyinyi.. [Al-Kahf: 110]

 

 

Hivyo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwa ni nuru na wala hakuumbwa kwa nuru, ila tu alikuwa kama watoto wengine wa Aadam isipokuwa tu Allaah Alimtofautisha yeye kwa ujumbe wa utume.

 

 

Imaamu waliotuhumiwa hawakutofautishwa kwa kitu chochote cha asili. Tamko la kwamba wao ni nuru kabla ya kuletwa (duniani), na kwamba wao wameizunguka ‘Arshi ya Allaah, ni kufru iliyo wazi na kupotoka kuliko wazi. Kama ingelikuwa haya ni kweli, ingeliingizwa ndani ya Kitabu cha Allaah na Sunnah ya Rasuli wake, lakini ni uongo wa kawaida ya waongo na wanafiki.

 

 

Kudharau watu na kuwanasibisha kwa Uungu ni kupelekea kwa kumshirikisha Yeye, Ametakasika Yeye kutokana na yale wanayomdai Yeye kuwa nayo. Yeye ndie pekee Aliyekuwepo (kabla) na hakukuwepo kitu chochote pamoja naye. Yeye ni wa mwanzo, kabla yake hakukuwepo yeyote, Yeye ni wa milele chini yake hamna yeyote, ametakasika kwa Rehma Zake. Ameviumba vyote kwa nguvu Zake na utukufu Wake, na kwa mnasaba wa uwezo Wake ni wa kusema “kuwa” linakuwa. Amemuumba Aadam kutokana na asili ya vitu vyote kwa kuunganisha kiume na kike. Hakuna yeyote kutokana na asili ya Aadam ambaye ameumbwa kwa nuru, wala hakuna yeyote (miongoni mwa binaadamu) aliyekuwa ni nuru kabla ya kuumbwa. Ni sawa na kusema, yeyote anayedai kuwa binaadamu ana njia ya (kujivua) visivyoonekana, ana uwezo wa kurekebisha shughuli zozote, ana uhakika wa kutoponyoka wala kuteleza, hana kasoro ya kusahau, ana elimu iliyo sawa na Allaah, na ana sifa kwa namna iliyo sawa na Allaah, ni kafiri asiyemuamini Allaah, na ni mnafiki ambaye anayetengeneza nje ya viumbe wanaoshindana na Allaah sawa na Yeye. Hakika Yeye Yupo mbali na yale ambayo wanamzulia.

 

 

4-Kutamka utukufu kwa wale wasio Rusuli, kuwatofautisha wao juu ya Rusuli na Manabii, ni kitendo cha kutoamini na unafiki, kwasababu Allaah Amechagua Rusuli na Manabii kutokana na binaadamu kwani Allaah Amewateua Rusuli na Manabii kuwaacha waumini wote inatambulika kwa dharura ndani ya dini, na inakubalika kwa Taifa la Kiislamu, umekataliwa tu na wanafiki ambao wanakataa upekee wa Allaah, haki na imani. Hivyo, madai kwamba ‘Aliy (Allaah Awe Radhwi naye), alikuwa ni bora kuliko Nabii Ibraahiym, Nuuh au Yuunus bin Matta, ni madai ya kutomuamini Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) aliyesema: “Haimpasi muumini kusema: “Mimi ni bora kuliko Yunus bin Matta.” Hairuhusiki kwa Muumini kujidai bora kuliko Yuunus bin Matta, Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ijapokuwa Allaah Anamaanisha kwa tabia yake alipowaacha watu wake na hamaki wakidhani Allaah hatompa adhabu kali, hata hivyo alimpeleka kwa watu tofauti. Allaah Anasema:

 

فَالْتَقَمَهُ الْحُوتُ وَهُوَ مُلِيمٌ ﴿١٤٢﴾

Basi samaki kubwa likammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa. [Asw-Swaffaat: 142]

 

Alilaumika kwa kuwaacha watu wake bila ya kutoomba ruhusa kutoka kwa Allaah:

 

فَنَبَذْنَاهُ بِالْعَرَاءِ وَهُوَ سَقِيمٌ ﴿١٤٥﴾

Basi Tukamtupa kwenye ardhi tupu ufukweni (alipomcheua samaki) naye akiwa mgonjwa. [Asw-Swaffaat: 145]

 

 

Hiyo ilikuwa ni adabu juu yake, na ni ujumbe mzuri kwa Manabii na Rusuli ambao ni rahisi (kupelekewa) onyo la upole na adhabu pale ambapo wametenda kinyume na namna walivyotarajiwa, hata hivyo waliweza kufikia cheo cha ubora mara dufu kuliko binaadamu wote, cheo ambacho hakiwezi kufikiwa na Muumini yeyote wa Rasuli, hata awe ni mchaji Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  wa aina yoyote. Hivyo, si ‘Aliy bin Abi Twaalib na kizazi chake wala wale waliobora kuliko wao, kama Abu Bakr na ‘Umar (Allaah Awe Radhwi nao), ni wenye ubora juu ya Rusuli, kwani Rusuli na Manabii ni walio bora kwa waumini kwa insaafu ya kuteuliwa na Allaah na kuteremshiwa wahyi. Hivyo kumfanya ‘Aliy au kizazi chake chochote bora kuliko Nabiy, Rasuli au kwa Malaika hakika ni kufru, kurtadi kwa kwenda kinyume na Kitabu cha Allaah, kwa Sunnah ya Nabiy wa Allaah, na makubaliano ya Ummah wa Kiislamu.

 

 

Inajulikana kwamba ‘Aliy mwenyewe hakupatapo kutamka wala watoto wake, (na) waumini. Isipokuwa, alisema: “Hakika mimi ni mmoja wa Waislamu.” Hakupatapo kujidai kuwa ni mbora kuliko Abu Bakr na ‘Umar. Jee atajipa vipi cheo cha kuwa juu ya Manabii na Rusuli na Malaika walio karibu? Hapana! Ni tuhuma za uongo zilizofanywa na waongo ili kuongeza kosa jengine la jinai kwenye kumbukumbu zao zilizo wazi dhidi ya waumini wachaji Allaah.

 

5-Al-Maqaam al-Mahmuud, au kituo kitukufu, kitamilikiwa na mtumwa mmoja wa Allaah, Rasuli wa Allaah, Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) aliyetangazwa na Allaah:

 

وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا ﴿٧٩﴾

Na katika usiku, amka uswali (tahajjud) kuisoma (Qur-aan); ni ziada ya Sunnah kwako Asaa Rabb wako Akakuinua cheo kinachosifika. [Al-Israa:79]

 

Al-Maqaam al-Mahmuud, au kituo kitukufu, ni nafasi pekee ya maombezi aliyotunukiwa Rasuli wa Allaah, Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) ambaye anamiliki kituo hicho na kitasifiwa na viumbe wote siku ya Hisabu. Pia ni daraja ya Peponi aliyotunukiwa mtumwa mmoja tu wa Allaah, ambaye ni Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) aliyesema: 

 

 

“Unapomsikia Muadhini rudia maneno yake (yaani wito wa Swalaah) kisha niswalie, muombe Allaah anitunukie kuingia kituo kitukufu chenye heshima kubwa; ni daraja ya Peponi. Ni lazima kimilikiwe na Mtumwa mmoja wa Allaah, ninategemea itakuwa ni mimi” [Muslim].

 

 

Hivyo, sio ‘Aliy wala watu wake wa nyumbani (Ahlu Bayt) watakaotunukiwa kituo kama hichi. Yeyote anayedai vinginevyo ni muongo asiye na imani (thabiti) ambaye ana madai ya uzushi kwamba ana mamlaka ya kuelewa mambo ya ghaibu, ambayo yamemilikiwa mahsusi na Allaah. Madai kama haya yana alama ya kufru iliyo wazi.

 

 

6-Matamshi ya kwamba Maimaamu waliotuhumiwa wana (sifa) pamoja na Allaah (Subhanahu wa Ta’aalaa), hadhi ya kipekee ambayo haipatikani na Malaika wa karibu au rasuli, ni matamshi ya uzushi, Ni wapi ndani ya Kitabu cha Allaah, au ndani ya Sunnah ya Nabiy wa Allaah inapatikana? Au yapo wapi maneno ya Maimaamu waaminifu walipozungumza hayo?

 

 

Jee ‘Aliy bin Abi Twaalib (Allaah Awe radhi naye), au yeyote (miongoni) mwa watoto wake wamchao Allaah na wakweli, waliojidai (kuhodhi) hadhi ya kipekee? Wapo tena mbali kutokana na uongo dhidi ya Allaah Mtukufu. Uongo huu hauwezi kutolewa na Muumin. Kwa sababu hadhi kama hiyo ipo ndani ya elimu isiyoonekana, yeyote anayedai elimu hii (kuwa nayo) ni muongo na asiye Muumini. Allaah Anasema:

 

قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ ﴿٦٥﴾

Sema: Hakuna katika mbingu na ardhi ajuaye ghayb isipokuwa Allaah. Na wala hawatambui lini watafufuliwa. [An-Naml:65]

 

Allaah Amemshushia yasiyoonekana (yaliyofichikana) kwa Nabiy au Rasuli wa Allaah pekee. Yeyote anayedai kwamba wahyi ulipokewa baada ya kifo cha Rasuli wa Allaah ni “Kaafir” na “Zindiyq”. Yeyote asiyeamini mwisho wa Utume na kushushwa mara kwa mara wahyi ni murtadi ambaye hamuamini Allaah na Rusuli Wake.

 

 

Fikra hizo hapo juu zinamaanisha matamshi yaliyofanywa na Khomeini ndani ya kitabu chake “Serikali ya Kiislamu” (Islamic Government), na kuthibitisha kwamba aliyozungumza si chochote ila ni ukafiri na uongo, kwa namna hiyo Wanazuoni wa Kiislamu wakamtuhumu kwa ukafiri na upotovu.

 

 

iii- Madai Yake Kwamba Mafundisho Ya Imaamu Wake Yapo Sawa Na Yaliyomo Ndani Ya Qur-aan, Kwamba Imaamu Wake Hawakosei Na Kwamba Usahaulifu Au Ujinga Upo Mbali Nao

 

Khomeini pia alisema ndani ya kitabu chake “Serikali ya Kiislamu” (The Islamic Government):

“Mafundisho ya Maimaamu ni kama mfano wa Qur-aan. Si tu juu ya kizazi kimoja, bali kwa kila mtu wa kila umri na sehemu mpaka siku ya Hukumu.”

 

Tamko hili lina sifa ya kutoamini (kufru) kwa vipengele vingi:

Ameyaweka maneno ya Allaah Mtukufu na yale ya binaadamu kwenye mizani moja. Maneno ya Allaah hayawezi kushindanishwa. Yanapatikana ndani ya Kitabu ambacho uongo hauwezi kujazika, na ambacho kitu chochote hakiwezi kuondolewa. Lakini maneno ya wengine na mafundisho yao yana sifa ya kubadilishwa, kuteleza na makosa.

 

 

Hakuna kitu chengine Allaah Alichoahidi kukilinda zaidi ya Ujumbe Wake uliofunuliwa na Rasuli Wake. Ama kwa wengine, hamna asiyekosea. Wanaweza kuwa sahihi au kukosea. Sio 'Aliy au yeyote katika watu wake wa nyumbani aliyekuwa ana sifa ya kutokosea, wala mafundisho yake hayakuwa sawa na yale ya Allaah. Kwa mfano, Al-Hasan mtoto wa ‘Aliy (Allaah Awe Radhwi naye), ambao Mashia wanaitakidi kuwa ni miongoni mwa Maimaamu wao, alihitalifiana na baba yake kwenye baadhi ya mambo. Khomeini mwenyewe anamtuhumu ‘Aliy (Allaah Awe Radhwi naye) kwa kukosea na kujishusha cheo pale alipokubali suluhu baina yake na Mu’awiyah (Allaah Awe Radhwi naye), na kujizuilia kuzungumzia kwa kile Khomeini na kundi lake kuuiita “Msahafu au Qur-aan ya Faatwimah” na kutouleta mbele. Pia anamtuhumu Al-Hasan kwa kosa la kujiuzulu na kumpatia uongozi Mua’wiyah, na makosa mengi.

 

 

Kilicho muhimu hapa ni kuonesha kwamba hao Imaamu walikuwa sio watakatifu kwenye kukosea katika mazungumzo na vitendo vyao, wala mafundisho yao hayakuwa sawa na ya Qur-aan kama Khomeini anavyodai. Walikuwa ni sawa na waumini wengine na wamchao Allaah, isipokuwa kwa yale yaendayo sahihi pamoja na Kitabu cha Allaah yanayotokana na mafundisho yao yanakubalika, na yale ambayo hayakubaliani (na Qur-aan) yatatupiliwa mbali, kwa ujumla kazi zinazokusanywa na waongo na zikachapishwa kwa kutumia majina ya Imaamu (wana lengo la) kukuza uongo na ukafiri baina ya watu.

 

 

Wamewaendea kinyume Imaamu wamchao Allaah kwa kughushi dhidi yao uongo kama vile kuwasingizia kuwa wamehodhi elimu ya ghayb (yaliyofichikana), na kwamba hamna chochote kutoka mbinguni au ardhini kilichofichika kwa wao. Wanadai kuwa wanamuingiza Peponi yeyote wampendae, kumtoa motoni yeyote wamtakae, kuzimiliki chembe (atoms) za Ulimwengu, kuwa na mamlaka ya kurekebisha mambo, kufa watakapopenda, na mengine mengi. Imaam watukufu wapo mbali ya misumari ya hao waongo. Allaah Awashushie laana yeyote anayezungumza uongo juu yao.

 

…/3

 

 

Share