Khomeini Ndani Ya Darubini - 5: Kikao Cha Khomeini Na Kundi Lake Kuhusiana Na Nabiy Mtukufu

Khomeini Ndani Ya Darubini – 5

 

Kikao Cha Khomeini Na Kundi Lake Kuhusiana Na Nabiy Mtukufu

 

Imeandikwa na Wajiyh Al-Madini

 

Toleo la Pili

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Leo Waislamu wanashuhudia machafuko mabaya kabisa katika kumbukumbu za sasa, (machafuko yenyewe ni) Mapinduzi ya Kishia ya Khomeini nchini Iran, pamoja na kuwa tayari kwao kuuangamiza Ulimwengu wa Waislamu kwa kutengeneza taifa mbadala lenye uchu. Kwa vile taifa hilo linatumia mikutano ya dini kama ni udhuru wa kuropokwa sumu yao na himaya ya itikadi zao mbovu, inatupasa (sote) kuelewa ukweli huu.

 

 

Mfunguo sita (Rabiul Awwal) ni miongoni mwa sababu inazotumia taifa la Khomeini mjini Tehran kuwadanganya Waislamu kwa kusherehekea siku ya kuzaliwa Rasuli Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kuwaongoza ovyo wale wenye imani ya kawaida na wale wajinga kuamini kwamba yeye Khomeini anampandisha cheo na kumuadhimisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Lakini ukweli ni kinyume chake (kwani) Khomeini na kundi lake wanampiga vita Rasuli wa Allaah na kumshutumu kwa kila aina ya uongo na tuhuma kama zinavyotakikana kwa imani zao. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameepukana na uongo wao. Kwa mujibu wa imani zao alikuwa ni haini, mjinga, mpuuzi na mnafiki, aliyeshindwa kisawasawa kuwasilisha ujumbe na kuwaongoza watu, na hafai kwa kazi aliyopangiwa. Wanadai kwamba amejikusanyia pamoja naye watu waovu kabisa, wajinga wa Kibedui (washamba), na kuwafanya wao ni washirika wake, wategemezi na wapenzi wake, amefunga ndoa na binti zao na akawapa binti zake kufunga ndoa. Matokeo yake hawakuwa na shukrani kwake yeye na hawakustahiki heshima hii. Wamebadilisha dini yake kwa kuzigeuza sheria zake, wakavunja wasia wake, wakateka nyara haki za familia yake, na kuutafuna urithi wake, na kukibadilisha Kitabu cha Allaah. Hizi ni baadhi ya imani za Khomeini na genge lake, kwa ufupi kama zinavyoelezwa hapa chini.

 

 

Khomeini amekuwa ni mwakilishi wa Shia, ijapokuwa madhehebu hayo yamefichwa na Taqiyyah [kuficha kile ambacho unakiamini] kwa muda mrefu, na amekwenda hatua refu zaidi kwa pumbao, na kunukuu maandishi ya imani zao.

 

 

Kwenye hotuba yake ya kuadhimisha Shaaban 15 (Nisfu Sha’aban), amedai kwamba Imamu wao atawafunika wote waliokuja kabla yake, akiwemo Rasuli wa Allaah aliyeshindwa. Matokeo yake, wanachuoni wa Kiislamu wakatoa majibu yao (fatwa) kumtuhumu Khomeini kwa ukafiri kwa kumdhihaki na kumtuhumu kwa dharau Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

Kwenye hotuba yake nyengine aliyoitoa ‘siku ya wanawake’ (tarehe 2/3/1986) anadai kwamba Jibriyl, amani iwe juu yake, ameshusha wahyi kwa Faatwimah (Allaah Awe Radhi naye), kwa siku 75 baada ya kifo cha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) , na kwamba ‘Aliy (Allaah Awe Radhi naye) alikuwa ni mwandishi wake. Kwa kudai huko, anarudia kwa yale ambayo Mashia wamenukuu vitabu vyao wenyewe kwamba wanayo Qur-aan ya Faatwimah, ambayo ni kubwa zaidi mara tatu kuliko yetu na haina herufi hata moja kutoka kwetu.

 

 

Hivyo, Khomeini ametoa mwangaza kwa yale yaliyofichwa na yaliyotuhumiwa kwa Faatwimah (Allaah Awe Radhi naye) kuwa ni mwenye hadhi kuliko Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa sababu Qur-aan ambayo aliipokea haikubadilishwa na ni kubwa zaidi mara tatu ukilinganisha na ya baba yake ambayo imebadilishwa.

Anadai kwamba wale ambao wanapigana chini ya viongozi wake nchini Iraq na nchi za Waislamu, na hueneza uadui kila sehemu duniani, ni wenye ujasiri, na zaidi, ni bora kuliko waliopigana pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

Kwenye kitabu chake “Kashf al-Asraar” Khomeini anaeleza “Kosa la kubadilisha Kitabu cha Allaah ambacho kwayo Waislamu wanawashtaki Mayahudi na Wakristo linasimamishwa tu dhidi ya Swahaba wa Rasuli wa Allaah.”

 

 

Anafafanua zaidi ndani ya kitabu hicho hicho, “ilikuwa ni rabii kwao (Swahaba wa Rasuli) kuzificha aya kutoka kwenye Qur-aan, isipokuwa kwa maandishi ya Allaah kwa kubadilishwa, na kuyaficha mbali na watu”.

 

 

Yule ambaye anadharau kwamba Khomeini na genge lake wanampa heshima na mapenzi kwa ukoo wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni mkosa. Ukweli ni kwamba wanaonesha kwa uongo ili kuficha uadui dhidi ya Uislamu, na kuthibitisha laana za Ummah wa mwanzo na wa mwisho, na kumpiga vita kila mwanachama aliyekuwemo kwenye Nyumba ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) waliounganisha Ummah wa Waislamu, au yeyote anayezungumzia vyema kuhusu Swahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

 

Katika (kuadhimisha) siku ya Ghadir [Mashia wanadai ni sehemu aliyotawazwa ‘Aliy na Nabiy ukhalifa baada yake!!) alimlaumu ‘Aliy (Allaah Awe Radhi naye) kwa kukubali mazungumzo kwenye vita vya Siffiyn, na al-Hassan kwa kuachia madaraka kwa Mu’awiyah. Pia amedai kwamba ‘Aliy (Allaah Awe Radhi naye) hakufanikiwa kusimamisha taifa la Kiislamu kama inavyotakikana, na kwamba sio yeye wala Nabiy, wala wale waliokuja baada yake, waliofanikiwa kuusimamisha Uislamu au kusimamisha taifa la Kiislamu, hali kadhalika uadilifu wa Allaah bado haujafanikiwa kusimamishwa.

 

Ni yeye tu (bila ya shaka!) kwa niaba ya Imamu asiyekuwepo aliyefanikiwa kusimamisha Serikali ya Kiislamu na uadilifu wa Allaah. Huo utawala wake anaojidai ni wa Kiislamu unawasukumiza maelfu ya watu kwenye vitanzi na vifungu, kuwaweka rumande mamia kwa maelfu na kuwapeleka jela.

 

 

Tumetaja awali kwamba Khomeini amekuja kuwakilisha mawazo ya Kishia na kuweka bayana kila ambacho kilifichwa na kukifanyia kazi katika Katiba ya Iran, ambapo Kifungu cha 5 kinasomeka:

 

“Kipindi ambacho Imamu wa 12 yupo kwenye stara, ndani ya Jamhuri la Kiislamu la Iran, uongozi wa shughuli na uongozi wa watu ni jukumu la mwanachuoni mtiifu na mchaji Allaah, anayafahamika muda wote, kuwa ni shujaa anayeongoza kwa uvumbuzi, ambaye idadi kubwa ya watu inamtambua na kumkubali kuwa ni kiongozi…..”

 

 

Kwa mnasaba wa Katiba hii, Khomeini amejiteua mwenyewe kama ni Imamu na Naibu wa Imamu asiyekuwepo, ambaye hakupatapo wala hatopatapo kutokea. Pia amemvumbua Ja’afar na mawazo yake kama ni dini ya taifa. ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) yupo mbali na kushirikishwa kwenye mstari huu wa mawazo haya. Hakupatapo kudai kwamba wahyi ulikuja kwake, au kwamba alikuwa ni mwandishi wa mkewe, wala hakudai kufurahia hadhi juu ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) au ya Abu Bakr na ‘Umar, achilia mbali juu ya kwamba (yeye yupo bora) kuliko Nabiy na Malaika. Hakuwahi kudai kwamba watakuwepo maimamu 12 kutoka kwenye kizazi chake, au kuita kundi lolote maimamu kumi na mbili, kumiliki Qur-aan iliyo tofauti na kubadilisha maneno ya adhana (wito wa Swalah). Wala hakuwapiga vita wale Swahaba waongofu kabla yake.

 

 

Isipokuwa, amejithibitisha kwa ubora wao kuliko yeye, na kuomba kukutana na Allaah akiwa ametenda mema kama ya ‘Umar. Ukweli ametangaza hadharani kwamba hakutatokezea tena mtu mwengine kama ‘Umar.

 

Hii ndio imani ya ‘Aliy bin Abi Twaalib (Allaah Awe Radhi naye), kiongozi wa wachaji Allaah, na jeshi lake na washirika. Hitilifau ilikuwa ni kwa al-Khawaarij, ambao walijitenga kivita na kumtuhumu yeye kutokuwa na imani, hivyo alipigana nao.

 

 

Ama kwa Mashia ambao Khomeini na genge lake wanajinasibisha, karne zote wanafuata imani ya kurithi, wakimfanya na kuwaheshimu Allaah namna sawa na watu wa Khosrans, wafalme wa Kipashia (Persian Kings) na wanaoabudia moto (wamajusi). Khomeini na genge lake ni vizazi vya Abdullah bin Sabaa. Mayahudi ambao wamerithika kuiharibu dini ya Waislamu, ambao walipata hadhira miongoni mwa makundi ya Wafursi na watu wajinga. Ndio wao waliosema kwa ‘Aliy “Wewe ni Allaah” kwa namna hiyo, aliwachoma moto, wakisema “Nimejitolea mhanga kwa ajili yako wewe, Rabb wangu, kwamba uridhike na mimi. Hivi sasa tunatambua uhakika, kwamba wewe ni Allaah, kwa sababu hakuna anayeadhibu kwa moto ila ni Allaah.” Wafuasi wao, waliokosa hisia, wakazirithisha mafundisho yasiyo sahihi kwa wale baada yao, badala yake wanachukia kila nafasi waipatayo kusukuma chuki zao kwa Waislamu na kumsuta Rasuli wa Allaah kwa siri na dhahiri.

 

 

Wanamtuhumu Nabiy wa  Allaah kwa kuwa muoga na aso na akili, kushindwa kumteua ‘Aliy (Allaah Awe Radhi naye) waziwazi kama ni mrithi wake mpaka (pale) Allaah Alipomtahadharisha.

 

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٦٧﴾

Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako. Na usipofanya, basi utakuwa hukubalighisha ujumbe Wake. Na Allaah Atakuhifadhi dhidi ya watu. Hakika Allaah Haongoi watu makafiri. [Al-Maaidah:67]

 

 

Wanadai kwamba niya hiyo hapo juu kiasili (originally) inasomeka kama ifuatavyo “…fikisha uliyoteremshiwa kuhusiana na ‘Aliy (Allaah Awe Radhi naye) …” Na walitafsiri neno ‘watu’ ndani ya aya kama kuwaelezea Abu Bakr na ‘Umar. Lakini wanadai Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ni muoga sana kuelezea kwao (watu), na kudhihirisha wasia na amri ya Allaah, wasije watu wakajikusanya kumpinga yeye!!

 

 

Angalia Khomeini na wafuasi wake namna walivyo wapuuzi, waso na akili, wakithubutu kumpaka matope Rasuli wa Allaah kwa hadhi iliyo chini kabisa! Kwa urahisi Waarabu waliweza kumtofautisha yeye na maadui na rafiki zake, haswa kama ameishi naye muda mfupi. Kwa haki, angelimtambua zaidi kwa vile ameishi nae muda wote wa maisha yake. Wale wanafiki (sio tu) wanagombana na Utume, lakini pia kwa uaminifu, uhodari na ufahamu wake kwa kuweza kukusanya kundi la wasioamini na wanafiki ambao walikuwa na shauku ya kumsubiri afe ili kuchukua kiti cha uongozi, kuiharibu Qur-aan, kuwakataa watu wake wa ukoo na kuwakatalia wao haki ya Uimamu!

 

 

Waislamu wanaweza kuona wenyewe namna tuhuma zilivyo kubwa dhidi ya Nabiy wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ni lipi baya zaidi kuliko kumpiga vita Rasuli wa Allaah? Hamna binaadamu aliyeweza kuwa na dozi (maelfu) ya uhusiano pamoja na Rasuli wa Allaah kama Abu Bakr, (Allaah Awe Radhi naye). Hamna mwanamke aliyempenda kama ni mke kuliko Aaishah, hata hivyo hajasalimika na uadui wa kundi ovu hili kwa kadri ya kufikia kumtuhumu Aaishah kwa unafiki na uzinifu, ambazo amesalimishwa nazo kwa maneno ya Allaah, Ambaye Ameiita lawama hio ni uongo kwa kusema:

 

إِنَّ الَّذِينَ جَاءُوا بِالْإِفْكِ عُصْبَةٌ مِّنكُمْ ۚ  ﴿١١﴾

Hakika wale walioleta singizo la kashfa; (kumzulia mama wa waumini ‘Aaishah  رضي الله عنها) ni kundi miongoni mwenu.… [An-Nuwr:11]

 

na Allaah Anaendelea kumuelezea Aishah kwa kusema:

 

أُولَـٰئِكَ مُبَرَّءُونَ مِمَّا يَقُولُونَ ۖ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ ﴿٢٦﴾

Hao wametakaswa na tuhuma za wanayoyasema, watapata maghfirah na riziki karimu. [An-Nuwr:26]

 

 

Wanafiki wanawaita Abu Bakr na ‘Umar ‘visanamu viwili vya Kikuraishi’ na kuwaita kwa mzaha ‘al-Jibt’ (uchawi) na ‘at-Twaghuwt (kila kinachoabudiwa asiyekuwa Allaah). Wamewataja ndani ya vitabu vyao wakisema. “Ewe Allaah, wape laana visanamau vya Kikuraishi, Jibt wao na Taghuwt wao na walaani mabinti zao.” Wakimaamisha wake wawili wa Nabiy: Aaishah binti wa Abu Bakr, na Hafsah binti wa ‘Umar.

 

 

Hao wazandiki wameridhika kumpiga vita na kumpaka matope Rasuli wa Allaah, lakini wanajua kwamba kufanya hivyo wazi wazi itawafanya Waislamu wote duniani kuwa dhidi yao. Hivyo, wanajitangazia kama ni wartadi na kurudia mara kwa mara kwa kufikisha hila za kumtuhumu kila mtu anayemzunguka Rasuli wa Allaah kwa kutoamini kupiga chenga na unafiki na kwa kufuata mawazo yao ya kigeni yenye kinyongo kwa ajili tu ya kupata ladha fupi ya dunia. Hivyo kumvamia Nabiy wa Allaah kwa mlango wa nyuma na kumfanya aonekane kama ni mtu asiye na thamani ambaye hafai kuwa ni Rasuli wa Allaah.

 

 

Tuhuma zinazofanywa kwa hao Wazandiki, kwamba Swahaba wote wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wamertadi isipokuwa watatu au watano, hapana shaka inamaanisha kuzikataa sifa muhimu za Nabiy; uongozi wake, usafi wake na uaminifu wake.

 

Allaah Amemsifu kwa kusema:

 

 

هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٢﴾

Yeye Ndiye Aliyepeleka Rasuli kwa wasiojua kusoma wala kuandika miongoni mwao anawasomea Aayaat Zake na Anawatakasa, na Anawafunza Kitabu na Hikmah na japo walikuwa hapo kabla katika upotofu bayana. [Al-Jumua’ah :2]

 

 

Kwenye ayah hii, Allaah Mtukufu, Anaukumbusha Ummah wa Waislamu kwa rehma ambazo Amewaneemesha juu yao kwa kumtuma kwa ajili yao Rasuli kuwasafisha na kuwaongoza. Pia Anamkumbusha Rasuli wake kwa kumpatia sifa ya kufaa kwa kazi hii kwa mnasaba wa Ummah wake ambao pia unafaa (kuwa na Nabiy huyo).

 

 

Kwa kusifiwa na Allaah, ina maana kuwa yeye ametimiza ujumbe wake kamili. Hivyo, hakuna nafasi ya shaka iliyoachwa kwamba ujumbe wake hakika ulikuwa na mafanikio kupita mpaka kwa kutimiza ujumbe, na kusimama Swahaba wazuri na wasafi hivyo kustahiki sifa zinazotoka kwa Allaah. Laiti Rasuli wa Allaah angelishindwa kazi yake, bila ya shaka Allaah Asingelimpatia amri yeye.

 

 

Lakini genge hili la wazushi, Khomeini na mfano wake, wanampinga Allaah na kuendelea kwa tuhuma zao na uongo, wakisema kwamba wote isipokuwa Swahaba wachache walirudi kutoamini. Hata ‘Aliy (Allaah Awe Radhi naye), ambae wanaamini kama ni mmoja kati ya watatu aliyebaki kwenye Uislamu, wanadai aliogopa kuuweka sawa uongo!!

 

 

Katiba ambayo Khomeini anaiita “Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu” inaegemeza mamlaka yote kwake yeye, bila ya kufuata Kitabu cha Allaah na Sunnah za Rasuli wake. Ukweli huu unasisitizwa kwa uwazi ndani ya Katiba ibara ya 5 kifungu cha 2 kinachosomeka:

“Uimamu na kiongozi anayefaa na mamlaka ya utambuzi yataendelea kuwa ni Mapinduzi ya Kiislamu.”

 

 

Uimamu ndio imani kuu ya dini yao. Sheria za Rasuli wa Allaah na Sunnah zake zinawekwa nafasi ndani ya Serikali ya Iran pamoja na Khomeini mwenye sheria ambaye ana mamlaka sawa kama ya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Mtunga sheria huyu ni mtoto aliye na umri wa miaka minne aliyeingia ndani ya tundu miaka 1200 iliyopita na hakutoka humo tena. Kwa jina la mtoto huyu, anatokea mtu anakuja kutawala, ambaye ni zaidi ya mpotovu, muovu, aliyejaa chuki na mwenye ulimi wa uongo kuliko mtu yeyote dunia hii iliyomshuhudia. Khomeini amemshinda kila mpiga vita aliyemvamia Rasuli wa Allaah na Swahaba zake waliosafi. Mtu huyu huyu hakosi nafasi ya kuwatukuza visanamu vyake, maadui wakubwa kabisa wa Rasuli wa Allaah: Nasr al-Deen al-Tuusi Mmajusi na Ibn al-Alqam, ambao walikuwa ni washauri wa Mumongoli Holaga ambaye aliongoza mauaji ya Waislamu Baghdad, Iraqi. Tukio lililoweka historia ya kumalizika Uongozi wa Abbasid. Leo wanafiki Iran wanaadhimisha siku ya kuzaliwa ya Nabiy kuwalaghai Waislamu kuamini kuwa wanampenda na kufuata Sunnah yake (Nabiy) na imani.

 

.../6

 

 

Share