05-Uswuul Al-Fiqhi: Sayansi Ambayo Uswuul Al-Fiqh Imepata Msingi Wa Elimu.

 

Sayansi ya Uswuul al-Fiqh hakika ni somo huru na la kiaina yake. Hata hivyo, limeegemea kwenye misingi mahsusi ya kutoa hoja fulani juu ya hoja fulani. Elimu ambayo wanazuoni wa Sheria za Kiislamu hawawezi kufanya kitu bila yake. Njia hizi za kutoa hoja juu ya hoja nyengine, zimetolewa kutoka katika adabu tofauti:

 

a)    Nyengine zimetolewa kutokana na sayansi ya dhana ya Aristotelia ambapo mwanafalsafa wa maandiko ya dhana mutakallimuun wamefikiria kuwa na desturi ya kujadiliana wanapoanza kazi zao. Majadiliano haya ya kielimu yanajinasibisha, kwa mfano, kwa taratibu ambazo ndani yake maneno yanatoa maana, mgawanyiko wa masomo kwenda wakati wa leo na kutabiri, haja ya, na aina za, maongezi ambayo yanaelemea kwenye kanuni za dhana zilizotolewa kutokana na tafsiri na maana. Usahihi na khitimisho zilizoegemezwa kwenye hoja ya kuongeza maarifa, na majadiliano kuhusiana na ushahidi na namna utakavyotumika kuthibitisha madai ya mmoja ambaye anathibitisha hilo, au kukanusha migongano na mengineo zaidi.

b)    Nyengine zimetolewa kutoka Ilm al-Kalaam Elimu ya akili na hoja, na inahusisha majadiliano ya masuala kama hayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu al-Haakim. Kwa namna ambayo ama ni Shari’ah hiyo hiyo au sababu zinazoamua lipi sahihi au lisilo sahihi, au ya kwamba ama mmoja anaweza kuwa na elimu ya zuri na baya kabla ya uteremsho (wahyi) au ama kutekeleza shukrani kwa Muumbaji Mwenye wingi wa ukarimu. Ni wajibu uliopatikana kwenye Shari’ah au sababu za mwanaadamu.

c)     Nyengine ni jumla ya kanuni za elimu ya lugha ambazo wanazuoni wa al-Usuul wameendeleza kupitia elimu na uchunguzi wa lugha na kuwasilisha kwa namna ya mfumo wa kudhihirisha. Kama vile uchunguzi unaohusisha lugha na asili zake, mgawanyo wa maneno kwenda kwenye kimafumbo na herufi halisi, majadiliano ya elimu ya asili, maneno mawili tofauti yenye maana sawa (utata), mkazo, ushauri wa juu juu, kuonesha uhalisia, maana ya vipande vya sarufi na mengineo zaidi.

d)    Njia nyengine zimetolewa kutoka sayansi bora ya Qur-aan na Sunnah. Kama vile mijadala kuhusiana na kupokewa Hadiyth kwa msimuliaji mmoja Ahaad, au kwa wasimuliaji wengi wasioweza kusimulia uongo Tawaatur, njia zisizokuwa rasmi za kuitafsiri Qur-aan na kanuni zake, utaratibu wa kuikubali Ta’diyl ama kuikataa Jarh ya wasimuliaji, kutangua sheria al-Naasikh wa al-Mansuukh[1], shuruti za maandiko ya Hadiyth na mfuatano wa wasimulizi, na mengineyo zaidi.

e)    Mwisho, mifano iliyotumika na wanazuoni wa al Uswuul kwenye ufafanuzi wa hoja zao. Ambazo zimetolewa kutoka kwenye Fiqhi maalum, na kutoka kwenye ushahidi wa kina kwa sababu hiyo hiyo kama ilivyochukuliwa kutoka kwenye Qur-aan na Sunnah.

 

Mambo ambayo wanachuoni wa al Usuul wanajishughulisha zaidi nayo, yanahusisha yafuatayo:

§         Elimu ya kuwaza kwa makini na kutoa habari fulani juu ya kitu fulani.

§         Elimu ya lugha.

§         Amri na Makatazo.

§         Maarifa ya kufahamu al-‘Aam na misamiati mahsusi al-Khaasw.

§         Mambo yasiyothibitika al-Mujmal na dhana zinazotambulika al-Mubayyan.

§         Kutangua an-Naskh.

§         Tabia (kwa uwazi, zile za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na maana zake).

§         Makubaliano.

§         Simulizi kuhusiana na Sunnah.

§         Kufatanisha hoja al-Qiyaas.

§         Kuelekeza hoja iliyo bora inapotokezea kesi zenye migongano zilio dhahiri.

§         Kutumia uwerevu wa akili na elimu Ijtihaad.

§         Kufuata madhehebu maalum ya kisheria Taqliyd.

§         Vyanzo vyenye mgogoro (ambavyo ni nje ya vile vyanzo vinne “vilivyokubaliwa”).

 

 

 

 [1] An-Naasikh wa al-Mansuukh: Ni somo la aya ambazo Qur-aan kwa maudhui yake zimetangua maana ya kisheria kwa aya nyengine, kwa hivyo inaitwa al-Mansuukh.Tawi hili la al-Uswuul pia linahusisha na somo la maudhui ya Hadiyth, aidha maudhui hayo yanaweza kutangua maana za kisheria ndani ya Qur-aan au kwenye Hadiyth nyengine.

Share