Faluda Katika Shepu Mbalimbali

Faluda Katika Shepu Mbalimbali

    

*Vipimo:

* Unaweza kufanya nusu yake

Majani ya faluda (rice grass) -  1/2  paketi

Maziwa -  7 gilasi

Sukari -  3/4 gilasi

Hiliki  ya unga -  1/4 kijiko cha chai 

Namna ya Kutayarisha na Kupika

1.  Katakata majani ya faluda uroweke kwa muda katika sufuria kwa maji kidogo sana.

2.  Tia maziwa katika hiyo sufuria iliyo na majani ya faluda na uchemshe huku unakoroga.

3.  Tia sukari.

4.  Endelea kukoroga hadi majani yayayuke.

5.  Epua kisha fanya ifuatavyo ukipenda kuyatia katika maganda ya mayai kama ilivyo katika picha.

Kutia faluda katika maganda ya mayai

1.  Unapotumia mayai, pasua yai juu kidogo tu utoe yai kisha uhifadhi maganda yake.

2.  Yaoshe maganda kwa maji ya moto na siki kidogo kuondosha harufu ya yai.

3.  Yapange maganda ya mayai katika boksi lake la mayai uweze kuyagandishia faluda.

4.  Gawa faluda sehemu tatu au zaidi upendavyo idadi ya rangi unazotaka kutia. Gawa katika bakuli.

5.  Tia kila moja rangi yake upendayo.

6.  Faluda ya wardi vizuri kutia sharbati ya rozi badala ya rangi lakini usitie tena hiliki hii.

7.  Nyinginezo zote tia hiliki kidogo.

8.  Mimina faluda katika maganda ya mayai uache igande katika mayai.

9.  Ikishaganda, menya kama unavyomenya mayai ikiwa tayari kuliwa.

Kidokezo:

Faluda ya rangi nyeupe ni bora kuigandisha katika chombo cha kawaida ili isije kuonekana kama yai hasa, kama tulivyofanya katika picha. Na uweza kupambia lozi hii nyeupe.

 

Share