Mikate Ya Ajemi

  Mikate Ya Ajemi

   

Vipimo

Unga - 3 mugs

Mtindi (yogurt) - 1 mug

Chumvi - 1 kijiko cha chai

Baking Soda - ¼ kijiko cha supu

Hamira - 1 kijiko cha supu

Mafuta - 3 vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya pamoja unga, chumvi, hamira, baking soda, mtindi na mafuta. Uchanganye unga na ukande uwe mlaini vizuri.
  2. Fanya madonge kama 8 kwa hicho kipimo cha  unga.
  3. Sukuma kila donge na upake samli na ukunje kama chapatti.
  4. Acha mpaka ikisha kuumuka. Sukuma duara isiwe myembamba kama chapatti iwe kidogo nene
  5. Choma kwenye jiko juu kama chapatti upande mmoja usigeuze. Epua  na uutie kwenye oven, uwashe moto wa juu mpaka uwe rangi ya hudhurungi (brown).
  6. Tayari kuliwa na chai au mchuzi au kitu chochote.
Share