29-Fatwa: Inaruhusiwa kuhamisha Zakaatul-Fitwr Kutoka Nchi Kwenda Nchi Nyingine?

 

Inaruhusiwa kuhamisha Zakaatul-Fitwr Kutoka Nchi Kwenda Nchi Nyingine?

 

 

SWALI:

Je, inaruhusiwa kutoa Zakaah kupeleka nchi nyingine ikiwa hakuna maskini nchi yangu? 

 

JIBU:

 

Sifa Zote Ni Za Allaah

 

Imesemwa katika Fataawa al-Lajnah ad-Daaimah 10/9:

"Zakaah itolewe kwa wale ambao Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amewataja kama Anavyosema: 

((Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanaozitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Allaah, na wasafiri. Huu ni waajibu ulio faridhiwa na Allaah. Na Allaah ni Mwenye kujua Mwenye hikima)) [At-Tawbah: 60].

Itolewe kwa Waislamu kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amemumbia Mu'aadh bin Jabal alipomtuma Yemen: ((Waambie kwamba Allaah Amewaamrisha sadaka (Zakaah) itolewe kutoka katika mali zao na itolewe kwa maskini wao)).

Maskini na wanaohitaji walio na ucha Mungu na wema ndio wanaostahiki zaidi kupewa kuliko wengine.

Hukmu ya asili kuhusu Zakaah ni kwamba itolewe kwa masikini katika nchi ambayo mali iko kutokana na Hadiyth iliyotajwa juu. Lakini ikiwa kuna haja ya kuihamisha kwengine kama nchi ambazo kuna masikini zaidi na mahitajio ni makubwa zaidi au ikiwa mtoaji anao jamaa zake ambao ni maskini n.k. basi inaruhusiwa kuihamisha.

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share