Zakaatul-Fitwr: Mke Yuko Mbali Na Mume, Zakaatul Fitwr Yake Itolewe Wapi?

Mke Yuko Mbali Na Mume, Zakaatul Fitwr Yake Itolewe Wapi?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

 mke ambaye anakaa mbali na mumewe lakini anahumiwa je zaka tulfitri yake itayolewa wapi na ninani mwenye jukumu la kutoa? Allaah Apokee ibada zetu.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himdi Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu Swalaah na salamu zimshukie kipenzi chetu Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Ikiwa mume ndiye mwenye kumhudumia mkewe na mke hana huna kipato chochote kingine basi mume ndiye mwenye kumtolea mkewe Zakaatul-Fitwr mahali ambako mali yenyewe ipo ya mtu mwenye kutoa.

 

Kwa maelezo zaidi bonyeza viungo vifuatavyo vya  Fataawa mbalimbali kuhusu hukumu za Zakaatul-Fitwr ambazo Alhidaaya.com imewatayarishia ile mpate majibu ya mas-ala yote mnayohitaji kuuliza na mzidishe elimu yenu.

 

Fataawaa: Za Zakaatul-Fitw

Fataawaa: Mukhtasari Wa Fataawaa Za Zakaatul-Fitwr

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share