Nangatai

Nangatai

 

Vipimo

 

Unga wa ngano  -  2 - 2 ¼ Vikombe

Siagi -  1 ½ Kikombe

Sukari  - 1 Kikombe

Yai -  1

Vanilla -Tone moja

Baking Powder -kijiko 1 cha chai

Chumvi   - Kiasi kidogo (pinch)

Unga wa Kastadi   - 2 Vijiko vya supu

 

Namna ya kutayarisha na kupika

  1. Changanya vitu vyote isipokuwa unga.
  2. Tia unga kidogo kidogo mpaka mchanganyiko uwe sawa.
  3. Kisha fanya duara ndogo ndogo uzipange kwenye treya na utie rangi katikati.
  4. Halafu zichome katika moto wa 300°F kwa muda wa dakika 20 - 25 na zisiwe browni .
  5. Kisha panga kwenye sahani tayari kuliwa na chai.

 

 

 

 

 

 

Share