Ukifanya Sajdatus-Sahw Unatoa Salaam Au Hutoi?

 

SWALI:

 je ukimaliza "Sijdatus-sahw unatoa Salaam au hutowi


 

 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na Salaam zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

Kwa hali zote mbili za kusujudu kwa kusahau ima kabla ya Salaam au baada ya Salaam, utatakiwa utoe Salaam baada yake. Usimulizi mbali mbali umetaja kufanya hivyo:

 

عن عَبْدَاللَّهِ بن بُحَيْنَةَ رضي الله عنه : أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم صَلَّى بِهِمُ الظَّهْرَ فَقَامَ فِي الرَّكْعَتَيْنِ الْأُولَيَيْنِ لَمْ يَجْلِسْ فَقَامَ النَّاسُ مَعَهُ حَتَّى إِذَا قَضَى الصَّلَاةَ وَانْتَظَرَ النَّاسُ تَسْلِيمَهُ كَبَّرَ وَهُوَ جَالِسٌ فَسَجَدَ سَجْدَتَيْنِ قَبْلَ أَنْ يُسَلِّمَ ثُمَّ سَلَّمَ متفق عليه

 

Kutoka kwa ‘Abdullaahi bin Buhaynah (Radhia Allaahu ‘anhu) kwamba: “Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam) aliwasalisha Adhuhuri akasimama katika rakaa mbili za mwanzo, kisha hakukaa (kikao cha mwanzo cha Tashahhud). Watu wakasimama naye hadi ilipomalizika Swalah wakasubiri atoe Salaam. Akatoa takbiyrah akiwa amekaa akasujudu Sajdah mbili kabla ya kutoa Salaam kisha akatoa Salaam” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Hivyo inapasa kutoa Salaam tena baada ya kufanya Sajdatus-Sahw.

Na Allah Anajua zaidi

 

Share