Kuadhini Na Kukimu Swalah Lazima Kila Swalaah?

 

Kuadhini Na Kukimu Swalah Lazima Kila Swalaah?

 

 

 

SWALI:

 

ASALAAM ALEYKUM TAFADHALI NAOMBA NISAIDIE SWALA HILI: JE NI LAZIMA KUADHINI NA KUKIMU KABLA YA KUSWALI?  

 

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Adhana na kukimu Swalaah ni mwongozo kutoka kwa Nabiy wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa tufanye hivyo kwa kila Swalaah isipokuwa kwa hali fulani. Inajulikana kwamba lengo la Adhana ni kuwajulisha Waislamu kuwa wakati wa Swalaah umekaribia.  Sasa  ikiwa tutaadhini Alfajiri pekee hizo nyakati nyengine watu watajuaje.   

 

Adhana inakuwa moja ikiwa kuna dharura inayoruhusika kishariy’ah kuunganisha  Swalaah mbili mfano ya Adhuhuri na Alasiri au Magharibi na ‘Ishaa.  Kutakuwa na adhana moja kwa Swalaah hizo mbili lakini iqaama zitakuwa mbili.

 

Kwa maelezo zaidi ingia katika kiungo kifuatacho:

 

 

Swalaah Ya Safari Inaadhiniwa na Kukimiwa?

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share