Supu Ya Adesi, Spring Beans Na Karoti

Supu Ya Adesi, Spring Beans Na Karoti

 

Vipimo

Adesi - 1 kikombe

Spring beans - 1 kikombe

Karoti - 2

Kitunguu - 1 -2

Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha chai

Nyanya - 2

Kidonge cha supu (stock) - 1

Chumvi - kiasi

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Ndimu au siki - 1 kijiko cha supu

Mafuta - 2 vijiko vya supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Katakata springbeans na karoti ndogo ndogo kiasi.
  2. Osha adesi na chemsha pamoja na spring beans na karoti hadi ziwive.
  3. Katika sufiria nyingine, tia mafuta, kaanga kitunguu kilichokatwakatwa hadi kianze kubadilika rangi.
  4. Tia thomu, kaanga kidogo tu kisha tia nyanya endelea kukaanga, tia chumvi, pilipili manga.
  5. Mimina supu ya adesi, springbeans na karoti, tia kidonge cha supu.
  6. Mimina vyote katika mashine ya kusagia (blender) usage kidogo tu.
  7. Rudisha katika sufuria, tia vipande vya karoti na springbeans kidogo tu, tia ndimu au siki na iache ipikike kidogo, ikiwa tayari.

 

 

 

 

 

 

  .

Share