Supu Ya Nyanya

Supu Ya Nyanya

Vipimo:

Nyanya ziilokatwakatwa (chopped) - 1.3 Kilo

Vitunguu vilokatwakatwa (chopped) - 2

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 3 chembe

Nyanya kopo (tomatoe puree) - 2 vijiko vya supu

*Supu ya kuku - 1 lita

Siagi - 10 gm

Mafuta ya zaytuni (olive oil) - 3 vijiko vya supu

Pilipili manga - ½ kijiko cha chai

Chumvi - kiasi

Kidokezo

* - unaweza kutumia vidonge vya supu na kutia maji ya moto  vikombe 4 ¼  vya maji kupata supu.

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Weka sufuria ya kiasi motoni na tia mafuta na siagi. Korogoa iyayuke.
  2. Kaanga vitunguu na thomu iliyosagwa au kuchunwa. Kaanga hadi igeuke rangi ya hudhurungi.
  3. Tia nyanya zilokatwa ndogo ndogo, nyanya kopo. Kaanga kidogo.
  4. Tia supu ya kuku. Koroga, funika kisha acha ichemke kwa muda wa robo saa.
  5. Acha ipoe, kisha mimina katika mashine ya kusagia (blender) isagike vizuri.
  6. Rudisha katika sufuria tia pilipili na chumvi ikiwa tayari.

 

 

 

 

 

 

 

Share