Nywele Zikitoka Na Kucha Zikikatika Je, Ihraam Inavunjika?

 

Nywele Zikitoka Na Kucha Zikikatika Je, Ihraam Inavunjika? 

 

Alhidaaya.com

 

 

Swali:

 

If I put the intention to slaughter , how does that work with the ihram that is, cutting the nails n hair. Because when I have to jitwahirisha (after haydh) i have to wash my hair and hair will come out. How will that work??. will my ihraam be invalidated? Please advice...

 

 

Jibu:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.IBU:

 

 

Hali ya kuwa katika ihraam kwa wenye kutia nia ya kuchinja ni Rahma ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa waja Wake ili wajihisi kuwa wako katika hali ya taqwa na wajihisi kuwa wanashiriki katika 'ibaadah za Mahujaji. Inapasa basi kuitumia neema hiyo kwa kujitahidi kubakia katika hali hiyo ya ihraam kwa kadiri mtu awezavyo.

 

 

Ikiwa umeosha nywele na zikang'oka wakati wa kuosha au wakati wa kuchana au ikiwa mtu kakata kucha kwa kusahau, yote hayo hayavunji Ihraam ya mtu. Lakini walioko Hajj wazingate sana kutokufanya makosa hayo kwani matendo mengineyo yaliyoharamishwa hupasa mtu kulipa fidia. Ama kwa hali ya muulizaji kuhusu Ihraam ndogo ya nje ya Hajj kwa ajili ya kuchinja hakuna fidia na kuchinja kwako kutakuwa kumekamilika In Shaa Allaah.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 
Share