Matatizo Ya Pesa Katika Biashara – Hataki Kulipa Pesa Za Aliyeshirikiana Naye

SWALI:

 

FAMILY TATU NI SHIRIKA KATIKA KAMPUNI. KUNA MWENGINE WA NNE MWENYE KUENDESHA KAMPUNI LAKINI SI SHIRIKA. MWENYE KUENDESHA KAMPUNI ANAMDAI SHRIKA MMOJA WA HIO KAMPUNI LAKI

SABA. WASHIRIKA HAO WATATU WANAMDAI HUYO MWENYE KUENDESHA KAMPUNI MILLIONI MBILI.

MWENYE KUENDESHA KAMPUNI HATAKI KUTOA HIZO MILLIONI MBILI MPAKA ALIPWE LAKI SABA ZAKE NA YULE MMOJA KATI YA HAO WASHIRIKA. SWALI LANGU NI WACHUKUE HATUA GANI WALE WASHIRIKA ILI WAPATE PESA ZAO. WAO WALIMWAMBIA MWENYE KAMPUNI AKATE PESA ZAKE KATIKA ZILE MILLIONI MBILI KISHA AWALIPE ZILIZO BAKI. HATAKI KUFANYA HIVYO.

AZAKUMULLAHU KHAYRA KWA WEBSITE HII TUNANUFAIKA KILA SIKU.

SISTER IN ISLAM

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako dada yetu. Hukutubainishia kuhusu hawa washirika na mwenye kuendesha kampuni wote ni Waislamu au wapo wasio Waislamu. Hata hivyo, tutajaribu kukupatia nasaha zetu kuhusu hilo kwa hali itakayokuwa.

Inaonekana awali ya yote hamkufuata kanuni za Uislamu zinazotaka mambo yetu na hasa yanayohusiana na pesa kuandikwa. Mikataba na maahidiano ni njia nzuri sana kuondoa migogoro ya baadaye. Biashara za ushirika ni lazima ziandikwe kwa njia ya kuondoa dhuluma baina ya washirika. Ilikuwa pia inatakiwa kuwa mwenye kuendesha kampuni ijulikane atapata nini, je atapata mshahara wa mwezi au atapata mgao katika faida. Ikiwa masuala hayo yameandikwa basi hamngekuwa na shida yoyote ile. Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Anasema:

Ila ikiwa ni biashara ya mkono-kwa-mkono baina yenu, basi hapo si vibaya kwenu msipoiandika. Lakini mnapouziana wekeni mashahidi. Wala asitiwe matatani mwandishi wala shahidi” (2: 282).

Inashangaza kuwa mwendeshaji kampuni hakukubali wazo la kukatiana hizo pesa kwani hiyo ndiyo iliyokuwa njia ya sahali kabisa. Haiulikani katika muamalati yeye ni mtu wa aina gani – ni muaminifu au si muaminifu. Lile jambo ambalo mnaweza kufanya ni kuahidiana na mwendeshaji kampuni yenu kuwa alete hizo milioni mbili siku ambayo mtakubaliana na mwenzenu naye alete laki saba siku hiyo hiyo.

Njia nyingine ambayo mnaweza kuitumia ni kutafuta waamuzi ambao wanakubalika na kila upande ikiwa mnataka suluhu basi itapatikana bila tatizo. Ikiwa hamkupata suluhisho la tatizo hilo lenu itabidi mfuate njia za kisheria ambazo zinatambulika hapo mlipo.

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share