Kababu Za Kuchoma Katika Vijiti

Kababu Za Kuchoma Katika Vijiti 

 

Vipimo

Nyama ya kusaga - 3 Lb

Kitunguu saumu (thomu/galic) - 1 kijiko cha chakula        

Tangawizi - 1 kijiko cha chakula

Chumvi - Kiasi

Kotmiri - 1 msongo

Bizari ya kababu -  ½ pakiti ya 100g

(Kabaab mix)                                              

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

  1. Saga nyama pamoja na kotmiri mara mbili iwe laini kuliko ya  sambusa.
  2. Tia kwenye bakuli na changanya na vitu vyote pamoja.
  3. Viringisha kwenye vijiti vya kuchomea na acha kama muda wa saa.
  4. Choma (bake) katika oven kwa moto wa 350◦c  mpaka zigeuke rangi na kuiva.
  5. Zikishaiva ziweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa na saladi, chips, mikate au wali.     

Kidokezo: 

  1. Ni bora kuviroweka vijiti vya kuchomea na maji usiku nzima ili ukichoma  kababu vijiti visiungue.
  2. Tumia bizari zako mwenyewe upendazo ikiwa huna hiyo ya Kabaab Mix.

 

 

 

 

Share