Vipapatio Vya Kuku Wa Kuchomwa (Grilled) Na Sosi Ya Nyanya

Vipapatio Vya Kuku Wa Kuchomwa (Grilled)  Na Sosi  Ya Nyanya 

    

Vipimo 

Vipapatio (Chicken wings)  - 1 Kilo

Pilipili ya unga nyekundu - 1 kijiko cha supu

Tangawizi ilosagwa  - 1 kijiko cha chai

Kitunguu saumu/thomu kilosagwa - 1 kijiko cha chai

Dania/coriander ya unga - 1 kijiko cha chai

Jira/cumin/bizari ya pilau ya unga - 1 kijiko cha chai

Garama masala (bizari mchanganyiko) - 1 kijiko cha chai

Nyanya ilokatwa ndogondogo (Chopped)  - 1

Nyanya kopo -  I kijiko cha supu

Siki (au ndimu)  - 2 vijiko vya supu

Chumvi - kiasi

Mafuta - 3 vijiko vya supu

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Osha vizuri vipapatio kwa maji ya moto, chumvi na haldi (bizari ya manjano kukata harufu ya kuku. Weka katika chujio vichuje  maji 
  2. Katika bakuli kubwa, tia viungo vyote isipokuwa nyanya, nyanya kopo na mafuta. Changanya vizuri.
  3. Weka mafuta katika kisufuria kidogo, kisha tia nyanya, chumvi kidogo, kaanga pamoja na nyanya kopo. Kisha changanya pamoja na mchanganyiko wa viungo sosi..
  4. Punguza sosi ya nyanya kidogo weka kando kwa ajili ya kumwagia mwishoni.  
  5. Mimina vipapatio katika bakuli la mchanganyiko wa sosi ya nyanya, kisha roweka  kwa muda wa masaa. 
  6. *Panga vipapatio katika treya ya kuchomea ndani ya oveni kisha wachome vipapatio kutumia moto wa juu (grilled) ukiwa unavigeuzageuza. Karibu na kuiva, mwagia sosi ilobakika na endelea kuchoma na kugeuzageuza hadi vipapatio viive.    
  7. Epua na viweke katika sahani ya kupakulia vikiwa tayari.  

Kidokezo:   

*Unaweza kuchoma vipapatio katika jiko la mkaa

 

Share