'Aaishah (رضي الله عنها): Ndoa Changa Ya Mama Wa Waumini -1

 

Ndoa Changa Ya Mama Wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) - 1

 

Imetafsiriwa na Naaswir Haamid

 

 

Ndoa ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ‘Aaishah bint Abi Bakr ambapo ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) alikuwa yungali ndani ya umri wa utoto imekuwa ni jambo la kufikiriwa na kupekuliwa kwa lengo la kutoa lawama ndani ya nchi za Magharibi. Bahati mbaya, ndani ya Miaka hii ya Ukoloni Mamboleo wa makombora yaliyo makini (kama vile MTV, CNN na Big Mac) wale ambao wanaojinasibisha kuwa ni Waislamu, wao wenyewe wamekuwa ni wenye kulaumu. Waislamu wengi, wanaokutana na hoja za kubomoa zinazodai “umoja” wa maadili ya ukombozi ya watu wa Magharibi, ambazo zimeenea takriban kwa kila mtu pembeni mwake, kwa fadhaa na upuuzi wanaacha kujadili yale masuala yanayoonekana ya ‘kutahayarisha’ ya Kiislamu.

 

Ni uchunguzi ulio sahihi na mwepesi kwamba ingawa nguvu za Ulaya zimeondosha majeshi yao ya kikoloni nje ya ardhi za Waislamu na kuwapatia “uhuru”, msiba mbaya zaidi bado unaendelea. Laana hii ni ya “Ukoloni wa Akili” na ulio hatari zaidi kwani ni ulio na hila nyingi zaidi. Insha Allaah, makala hii itakuwa na mchango wa kuwafanya Waislamu na wasiokuwa Waislamu ujuzi wa sio tu malengo sahihi kuhusiana na ndoa ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha), lakini namna ya kuielewa kwa kutumia nuru ya Uislamu na maisha ndani ya ulimwengu wa “kisasa”.

 

Kwa masikitiko, wale miongoni mwetu tunaojaribu kueneza ukweli wa Uislamu ndani ya nchi za Ki-Magharibi, mara kadhaa tunalazimika kukubaliana na mwenye elimu ya nchi za mashariki W. Montgomery Watt pale alipoandika: “Katika watu wote maarufu, hakuna ambaye amekuwa ni muovu zaidi kama Muhammad.[1] Lakini hapa, kwa kuleta mabadiliko, tunajadili kitu ambacho ni sehemu ya ukweli wa taariykh ya Uislamu, sio tukio la uongo au uzushi ambalo watu wa Magharibi wametumbukizwa ndani yake kuamini kuwa ni kweli, kama vile tukio linalodai kuitwa “Aya za Kishetani”. Kwamba mtu wa umri wake wa miaka ya hamsini atakwenda kumuoa mwanamke mdogo – haswa mtu ambaye anayetarajiwa kuwa ni mfano wa maisha yenye ustaarabu – sio kazi ngumu tu kwa watu wa Magharibi wa “kisasa” kukutana na misamiati hiyo, lakini pia hali imekwenda mbali zaidi hadi kuchanganya tuhuma za kuchefua za “mwenendo wa kujamiiana” miongoni mwao. Kwa uoni wa fedheha kama hizo, Waislamu mara zote hawakuwa ni wenye kujibu vizuri.

 

Ndani ya karne iliyopita, ambapo Waislamu wengi walikuwa “Wameleweshwa kwenye Umagharibi” na wapo tayari kufanana na tumbili kwa kuwafuata Wazungu takriban kwenye kila kitu, urejeo uliokuwa wa kawaida ni kukataa vyanzo vilivyosimulia dai “la tatizo linalofedhehesha”. Kwa Waislamu wa “kisasa”, wanaojadili kwamba ni hukumu PEKEE inayopatikana ndani ya Qur-aan ndio halali Kiislamu, wakifuta pembeni nyanja hii ya maisha ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa njia nyepesi. Bila ya kuona taabu, walikataa kwamba ilitokea na kuvishambulia vyanzo ambavyo vimesimulia.

 

Matokeo yake kwa Waislamu, hadi leo hawa “Warushaji makombora juu ya Uislamu” hawajakubali makosa yao na wamepotea ndani ya kizingo kwa hatua kubwa mno. Hata hivyo, bado wapo Waislamu wengi huko nje wanaojaribu kuficha kwa yale wanayoyaona kuwa ni tatizo kwa kukataa vyanzo sahihi vya Kiislamu wakati huo huo wakijidai kuwa ni wafuasi wa Waislamu wa Ahl as-Sunnah (kimsingi yenye maana ya “Imani barabara ya Kisunni”, kwa wale wasioelewa vyema msamiati huo wa Kiislamu). Waislamu wengine wengi bila ya shaka bado wanawaza iwapo simulizi hiyo ni sahihi na namna ya kuielewa kama hasa ni kweli.

 

Ushahidi Wa Kiislamu Kuhusu Umri Wa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘Anha)

 

Kutokana na ujinga ulio wazi wa Waislamu wengi, labda kutokana na kusoma maandiko ya udhuru wa “kisasa” kama yaliyoelezwa hapo juu, ni vyema sasa tukaangalia vinasemaje vyanzo vya Kiislamu vilivyo sahihi kuhusu umri wa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) kuolewa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa njia hii, kabla ya kuendelea kwenye uchambuzi wa hoja za kweli, kwanza tutaweka wazi ni zipi hoja za Kiislamu zilizo kweli.

Kwenye nukta hii, ni bora kueleza kwamba ni sababu isiyo na mashiko inayotokana na msimamo wa Kiislamu kusema kwamba umri wa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) “haupatikani ndani ya Qur-aan”, kwani vyanzo vya maandiko ya Uislamu yanaunganishwa PAMOJA kwa Qur-aan na Sunnah, na Qur-aan inatuambia hivyo. Kwa wale wanaotaka (au wenye haja) ya kusoma zaidi kuhusu nafasi ya Sunnah ndani ya Uislamu, tafadhali soma Utangulizi wa Sunnah - An Introduction to the Sunnah na/au Sunnah na Nafasi Yake Ndani ya Sheria Za Kiislamu – The Sunnah and Its Position in Islamic Law.

 

Sasa kwa mtazamo wa namna vyanzo vya Kiislamu hakika vinavyosema, inaweza kufikia hatua ya kukasirika kwa baadhi ya Waislamu “wa kisasa” na “wa utamaduni” kwamba kuna ahaadiyth nne ndani ya Swahiyyh al-Bukhaariy na ahaadiyth tatu ndani ya Swahiyh Muslim ambazo zinaeleza wazi wazi kwamba ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) alikuwa “umri wa mika tisa” wakati ambao kwamba ndoa yao ilikamilika kwa kitendo cha ndoa baada ya kuoana na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ahaadiyth hizi, ambazo zina tofauti ndogo, zinasomeka kama ifuatavyo:

‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha), amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alifunga ndoa (zawaaj) naye akiwa na umri wa miaka sita na kuitimiza ndoa yake kwa kitendo cha ndoa (nikaah) akiwa na umri wa miaka tisa, na baadaye alibaki naye kwa miaka tisa. (Swahiyh al-Bukhaariy, Juzuu ya 7, Kitabu 62, Nambari 64).

 

Kati ya ahaadiyth hizi ndani ya Swahiyh al-Bukhariy, mbili zimesimuliwa kutokana na ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) (7:64 na 7:65), moja kutokana na Abu Hishaam (5:236) na moja kupitia kwa ‘Ursa (7:88). Ahaadiyth zote hizo tatu ndani ya Swahiyh Muslim zina ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) kama ni msimuliaji. Kwa kuongezea, ahaadiyth zote ndani ya vitabu vyote hivyo viwili zinakubaliana kwamba ndoa hiyo ilifungwa mkataba wa kindoa pale ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) alipokuwa “umri wa miaka sita”, lakini haikukamilishwa (kwa tendo la ndoa) mpaka alipofikia “umri wa miaka tisa”. Kwa kuongezea, hadiyth ambayo kimsingi ina maandiko sawa (matn) inasimuliwa ndani ya Sunan Abi Daawuud.

 

Wala hakuna haja ya kusema, ushahidi huu – kuzungumzia Kiislamu – kwa hadhi ya juu kabisa ni yenye nguvu, na Waislamu wanaoukataa, wanafanya hivyo kwa malengo tu ya kuharibu hadhi yao ya kielimu, imani safi au vyote. Kuwekwa wazi kwa ushahidi huu, kumeonesha kwamba hakuna haja ya ziada ya kufanya mjadala kuhusu umri wa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) miongoni mwa waumini Waislamu. Labda mtu athibitishe kwamba ndani ya lugha ya Kiarabu “umri wa miaka tisa” ina maana ya kitu chengine kisichokuwa “umri wa miaka tisa”, hivyo ni lazima sote tuwe na msimamo ndani ya imani zetu kwamba alikuwa na “umri wa miaka tisa” (kana kwamba kuna hoja au haja ya kuamini vyenginevyo?!).

 

Juu ya ukweli huu, bado kuna baadhi ya waandishi Waislamu ambao kwa namna fulani wameweza kuusukuma umri wa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) nje hadi umbali wa “umri wa miaka kumi na nne au kumi na tano” wakati wa ndoa yake kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hata hivyo, kwa hapa wala usipatikane mshangao wowote, kwani hakuna hata mmoja wao aliyetoa thibati, ushahidi au nukuu kwa maoni yao. Hili linaweza kuzungumzwa kwa kujiamini mno, kwani uhakika hakuna hata mmoja anayeweza kutoa vyanzo vilivyo sahihi zaidi kuliko mkusanyo wa hadiyth za Imaam al-Bukhaariy na Muslim!

Kwa kuegemea na uchunguzi ambao nimeufanya. Ninahisi kwamba kuna chanzo kinachofanana kwa wale wanaodai kwamba umri wa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) wakati wa ndoa hiyo ulikuwa “umri wa miaka kumi na nne au kumi na tano”. Chanzo hichi ni “The Biographies of Prominent Muslims” - “Maandiko ya Habari za Maisha ya Waislamu Mashuhuri” ambacho kimechapishwa kwa mtindo wa kitabu, kwa CD-ROM na imewekwa sehemu tofauti kwenye mtandao. Mfano mwengine tu wa kwanini kwenda katika vyanzo ni muhimu...

 

 

Inaendelea ..../2

 


 

[1] W. Montgomery Watt, Muhammad at Medina-Muhammad Akiwa Madiynah, Oxford University Press, 1956.

 

 

Share