Tashahhud Kama Ilivyofundishwa Na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم)

 

SWALI:

naona msadaa wenu kuhusu atahiyatu kwa sani yenu kama hawezekani kukunijibu naona munambia nitafute njia nyengine ya kupata msadaa niliomba nindikiwe atahiya kwa kiswahili ya sunni na ya ibaadhi.

 


 

 

 JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Tunashukuru kwa swali lako, lakini tunapenda kukujulisha kwamba mafunzo ya Dini yaliyo sahihi ni kufuata Qur-aan na Sunnah na sio kufuata makundi fulani. Na hilo ndilo lengo la Alhidaaya kuwafunza mafunzo yaliyo sahihi tu yanayotokana na Qur-aan na Sunnah bila ya kuegemea kundi lolote lile.

Kwa hiyo hatuwezi kukusaidia kukupatia mafunzo yoyote mengine ya makundi fulani kwani itakuwa ni kukupoteza na mafunzo sahihi ya Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) badala ya kukuongoza.

Pia tunakushauri daima ukiuliza au ukitafuta jambo la Dini, uwe unauliza Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kasemaje au kafanyaje, na sio Ibadhi wamesema nini au Masuni wamesema nini! Siku ya Qiyaamah hutoulizwa kuhusu Uibadhi au Usuni au madhehebu yako uliyoyashikilia na ukaacha kumfuata Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kikamilifu kwa yote aliyokuja nayo.

Chukua mfano mzuri tu ulio hai, pale utakapoingia kaburini na kujiwa na Munkar na Nakiyr, utakapoulizwa maswali, utaulizwa ni ipi Dini yako? Na hutoulizwa ni lipi dhehebu lako!?

Hivyo, ni muhimu kushikamana na Uislam kama ulivyokuja kutoka kwa Mtume na kuacha taasubu za kukumbatia madhehebu. Na kama una ulazima wa kujinasibisha na madhehebu, basi fuata madhehebu ya Maswahaba ambayo hujulikana kuwa ni Ahlus Sunnah Wal Jama’ah (yaani Walioshikamana na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na nyendo za Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum)).

 

Mafunzo Swahiyh ya Swalah yanapatikana katika viungo vifuatavyo:

Mafunzo Swahiyh Ya Swalah

 

Vile vile Kitabu kifuatacho ambacho bado hakikukamilika kina mafunzo ya Swalaah kama alivyoswali Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa alihi wa sallam).

 

Swalah Ya Mtume (صلى الله عليه وسلم) Kutoka Mwanzo mpaka mwisho Kama kwamba unaiona

 

Endelea kufuatilizia kila wiki tunaweka mada mpya hadi kitakapomalizika utapata mafunzo kamili ya Swalaah.

Pia bonyeza viungo vifuatavyo upate kitabu kilicho na mafunzo ya Du’aa na Adhkaar pamoja na mafunzo ya Swalah yote pamoja na namna ya kusoma Tashahhud kama ilivyofundishwa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

Hiswnul Muslim

 

23 Dua'a Ya Tashahhud

 

24 Kumsalia Mtume صلى الله عليه وسلم Baada Ya Tashahhud

 

25 Dua'a Baada Ya Tashahhud Kabla Ya Salaam

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share