Chila 1

Chila - 1

   

Vipimo

 

Mchele -  2 Vikombe 

 

Tui  -  2 Vikombe 

 

Sukari - 1 Kikombe 

 

Maziwa -  ½ Kikombe 

 

Hamira - 1 Kijiko cha chai 

 

Hiliki - Kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

 

  1. Roweka mchele na maji kwa muda mpaka ulainike kiasi. 
  2. Chuja mchele kisha saga vitu vyote vilivobali katika mashine ya kusagia (Blender)  huku ukimimina tui kidogo kidogo mapaka limalizike 
  3. Mimina kwenye bakuli kisha acha  mpaka uumuke 
  4. Weka chuma cha kuchomea katika moto, kisha chota upawa wa mchanganyiko huo umimine kwenye chuma cha kuchomea huku ukiuzungusha utandazike. Choma katika moto wa kiasi. 
  5. Ukishabadilika rangi tu chini na ukafanya matundu matundu juu utoe na  weka kwenye sahani zikiwa tayari.

 

 

 

Share