Puri

Puri

Vipimo

Unga - 3 Vikombe

Mafuta ya zaituni au ya kawaida - ¼ kikombe

Chumvi - kiasi

Maji ya dafu dafu - ½ kikombe takriban

Mafuta ya kukaangia  katika karai

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Changanya vitu vyote katika bakuli, kisha ukande unga uwe kama wa chapati.  Ikibidi uongoze maji au unga ongeza kwani inategemea na mafuta utakayotumia.
  2. Fanya madonge madogo madogo, kisha yafunike kwa kwa mfuko wa plastiki au kitamba yasipate upepo kwa muda wa dakika 15-20
  3. Pasha moto mafuta huku unasukuma madonge yawe kiasi tu.
  4. Kaanga madonge ukitia moja moja au mawili mawili inategemea na ukubwa wa karai. Kaanga hadi yafure na kubadilika rangi.
  5. Epua na yatie katika chujio yatoke mafuta yakiwa tayari kuliwa.
  6. Kidokezo:
  7. Puri nzuri kuliwa na kuku wa kuchoma na sosi zake kama sosi ya ukwaju .

 

 

Share