B.B.Q Ya Slesi Za Nyama Ya Kondoo

B.B.Q Ya Slesi Za Nyama Ya Kondoo 

 

 

 Vipimo  

*Slesi Za Nyama ya Kondoo - 2 Kilo 

Kitunguu saumu/thomu na tangawizi iliyosagwa - 2 vijiko vya supu  

Pilipilimbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu 

Sosi ya HP au ukwaju - ½  kikombe 

Siki - 2 vijiko vya  supu 

Chumvi - kiasi 

Mdalasini wa unga - kijiko cha chai 

Jiyrah (cumin, bizari ya pilau ya unga) - 1 kijiko cha chai  

Pilipilimanga ya unga - 1 kijiko cha chai  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

  1. Changanya viungo vyote vizuri katika bakuli, kisha tia slesi za Kondoo, ziroweke kwa muda wa masaa katika friji au tokea usiku. 
  2. Baada hapo, changanya tena vizuri kabla ya kuchoma. 
  3. Pika katika jiko la B.B.Q au weka katika treya upike katika oveni kwa moto wa juu (grill) mdogo mdogo. 
  4. Geuza zinapowiva upande mmoja, choma upande wa pili, zikiwa tayari epua weka katika sahani zikiwa tayari.   

Kidokezo:  

*Slesi za nyama zikatwe kiasi na ziwe za mafupa kidogo.

  

 

Share