Kuku Wa Kuokwa (Baked Chicken)

Kuku Wa Kuokwa (Baked Chicken
 
Vipimo:
 
*Kuku mzima - 1
 
Tangawizi na kitunguu saumu/thomu iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
 
Mtindi - 3 vijiko vya supu
 
Rojo la ukwaju - 2 Vijiko vya supu
 
Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
 
Chumvi - kiasi
 
Bizari ya jiyrah (cummin powder) - 1 kijiko cha chai
 
Bizari ya dania (coriander powder) - 1 kijiko cha chai
 
Paprika -  1 kijiko cha chai
 

Hiliki   -  1/2 kijiko cha chai

Mdalasini -  1/2 kijiko cha chai
 
Siki au ndimu - 3 Vijiko vya supu
 
 * Ukipenda muache na ngozi bila ya kumchuna au mtoe ngozi.
 
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

  1. Changanya tangawizi na thomu, pilipili mbichi pamoja na vitu vyote vingine katika kibakuli.
  2. Mpasue kuku kidogo (slit) kila mahali kuweka njia ya kuweka huo mchanganyiko wa rojo la kuvumbika.
  3. Mtie hilo rojo kila sehemu na muacha avumbike (marinade) kwa muda wa masaa mengi katika friji.
  4. Paka mafuta kidogo katika treya umuweke kuku, kisha mchome katika oveni moto wa 450º kwa muda wa dakika 45 hadi awive.
  5. Mtoe na umuweke katika sahani ya kupakulia ukipambia na saladi upendavyo.

 

 
                                                         
 

 

Share