Mume Ana Ukimwi, Alimtoa Mke Katika Ukiristo, Mke Kajua Dini, Lakini Mume Kamkatisha Tamaa Kwa Kukosa Maadili Na Uaminifu

 

SWALI:

 

Assalaamu 'alaykum

swali langu ni Mimi nimeolewa na  nilikuwa Mkristo na kuslimu baada ya kutaka kuolewa na mme wangu ambaye ni Mwislamu,  na mimi nikajitahidi kufuata dini jinsi inavyotakiwa kima vazi (Hijaabu), swala mara 5, swala za usiku, kujifunza kusoma Qur`an mpaka Mwenyezi Mungu akaniwezesha na kuanza kuwafundisha watoto wangu kidogo dogo.

Mme wangu kwa bahati mbaya akaanza kuumwa ugonjwa  mbaya ukimwi inasikitisha sana (MWENYEZI MUNGU ANIEPUSHE NAO). NA MIMI HAKUNIAMBIA KAMA AMEATHIRIKA ALINIFICHA, LAKINI MWENYEZI MUNGU ALINIONGOZA NA KUTIA HOFU NA KUAMUA MWENYEWE KUPIGA SIMU HOSPITAL NDIO DAKTARI WAKE AKANIAMBIA INAPASHWA NA MIMI NICHUNGUZWE AFYA YANGU, DOCTOR HARUHUSIWI KUSEMA ANASUMBULIWA NA NINI ILA NA MIMI PIA INAPASHWA NIKACHUNGUZWE.

NIKAENDA NA MIMI KUCHUNGUZWA AFYA YANGU  NA NIKAONEKANA SINA (NEGATIVE) NA NIKAAMBIWA NIENDE TENA  BAADA YA MIEZI SITA . CONTROL YANGU IKAWA TENA SINA (NEGATIVE), SASA NIMIMALIZA.

SASA DAKTARI WANGU ALINIAMBIA SIO LAZIMA KUMUACHA LAKINI NITUMIE KONDOM;  LAKINI MIMI SASA SITAKI TENA NAYE TENDO LA NDOA HATA KAMA ATATUMIA CONDOM NIKIFIKIRIA TU UKIMWI SINA HAMU KABISA.  KWANI NASHIKWA NA UOGA. NA SASA NIMEJITENGA CHUMBA.

(1)  SASA JE NIKIENDA KWA SHEHE KUOMBA TARAKA JE NI DHAMBI?

(2)  AU NITAMUAIBISHA?

HUYU MME GANI KUONYESHA MFANO KAMA HUU KWANGU, UKIANGALIA ALIKONITOA KWENYE DINI NYINGINE?

NISAIDIENI NIPATA KUJUA KWANI SIFAHAMU KABISA NA INAPASHWA NIJUE ILI HATA WATOTO WANGU NITAWAFAHAMISHA.

Ahsanten,
 


 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mahusiano kwa wakati huu na mumeo.

Mwanzo tunakuombea sana katika mtihani ulionao kwa sasa uweze kuupita na kubaki na Imani mpaka uage dunia ukiwa katika hali hiyo.

Kwa hali uliyo nayo tunataria kuwa utakuwa na daraja kubwa mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Ni ajabu kuwa mume ambaye ni Muislamu ataasi na kumuacha aliyesilimu kumshinda katika Imani na matendo mema. Hata hivyo, mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) hakuna ajabu na aliyeingia katika Uislamu akiwa mtu mzima anaweza kuwa na daraja kubwa kuliko aliyezaliwa katika Uislamu. Na tunatarajia kuwa wewe utafikia daraja hiyo na zaidi.

Ama kuhusu migogoro au sintofahamu kwa wanandoa, Uislamu umeweka njia ya kuweza kutatua ili kama mlivyooana kwa jina la Allaah na kwa wema muachane kwa ihsani na wema. Hakika ni kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Amekulinda sana usiambukizwe ukimwi na mumeo ambaye anao. Hivyo unatakiwa uwe katika tahadhari usije ukakutana na mumeo kimwili usije ukashikwa na ugonjwa huo mbaya.

Nasaha ambazo tunaweza kukupatia ni kama zifuatazo:

1.    Kabla ya kuchukua hatua yoyote ni lazima kama wanandoa ukutane na mumeo na umueleze uliyonayo moyoni. Katika hili hakuna kuaibishana bali ni kuokoa maisha yako na kumweka yeye katika tahadhari kubwa sana. Inatakiwa uwe wazi sana katika hilo na itoke wazi kabisa rai yako kuwa ni bora kwa hali mliyonayo yeye mumeo akuache. Au ikiwa wewe ni mzee kiasi si rahisi kupata mume mwengine muwe mtaishi pamoja bila ya kukutana kimwili.

2.     Ikiwa suluhisho limepatikana itakuwa kheri kwenu nyote, lau ikiwa amekataa basi itabidi uite wawakilishi wake, na wako na wewe na yeye muwepo katika kikao. Kwani jambo hilo likitokea huenda ndio ikatokea aibu kwa mumeo kwani aliona kuwa ni siri yake na daktari wake lakini hakutakuwa na budi kufanya hivyo. Ikiwa kutapatikana suluhisho itakuwa kheri na lau hakukupatikana suluhisho lotote, itabidi uendelee mbele katika hatua nyingine.

3.     Itabidi uende kwa Qaadhi au Shaykh, kujieleza yako naye mumeo ataitwa kuja kujieleza na kisha hukumu kutolewa. Magonjwa yasiyotibika kwa upande wa mume ni sababu ya kuweza kumfanya Qaadhi kuwaachisha wanandoa.

Tunakutakia kila la kheri katika mtihani wako huo.

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share