Kuna Du'aa Maalumu Za Kujitwaharisha Janaba Hedhi Au Nifasi?

Kuna Du'aa Maalumu Za Kujitwaharisha Janaba Hedhi Au Nifasi?

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Assalam Aleikum

naomba tafadhali unisaidie na Dua ya Janaba na piya Dua ya Hedhi (wakati wa kujitoharisha).

shukran

ma'asalaam

 

 

 

JIBU:  

 

 

بسم الله، والحمد لله، والصلاة والسلام على أشرف الأنبياء والمرسلين نبينا محمد صلى الله عليه وآله وسلم وعلى آله وصحبه ومن اهتدى بهداه

Hakuna uthibitisho wowote katika mafundisho ya  Sunnah ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  kwamba kuna du'aa khaswa ya janaaba au ya hedhi au ya nifaas, ila tu anapofanya wudhuu hutamka:

بِسْمِ الله

 

BismiLLaah

 

kutokana na Hadiythi ifuatayo.   

 

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:   ((Hakuna wudhuu kwa asiyetaja jina la Allaah))    [Abuu Daawuwd]

 

Na kwavile ghuslu (josho) huanza mtu kwa wudhuu basi inafaa kuanza kwa kusema  

بِسْمِ الله

 

Ama baada ya kutoka kufanya wudhuu imethibitika du’aa ifuatayo:

 

أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ  

Ash-hadu an laa ilaaha illa-Allaah, Wahdahu laa shariyka Lahu wa ash-hadu anna Muhammadan ‘Abduhu wa Rasuwluhu

 

Nashuhudia (kwa kuamini moyoni na kukiri) kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila ni Allaah, Peke Yake, wala Hana mshirika, na ni nashuhudia (kwa kuamini moyoni na kukiri) kwamba Muhammad ni mja wake na ni Rasuli Wake.

 

[Hadiyth ya ‘Uqbah bin ‘Aamir Al-Juhniy(رضي الله عنه)     Muslim (1/209)]

 

  

 اللَّهُمَّ اجْعَلْنِي مِنْ التَّوَّابِينَ وَاجْعَلْنِي مِنْ الْمُتَطَهِّرِينَ

Allaahummaj-’alniy minat-ttawaabiyna waj-’alniy minal mutatwahhariyn

 

Ee Allaah, nijaaliye niwe miongoni mwa wenye kutubu na nijaalie miongoni mwa wenye kujitoharisha   

[Hadiyth ya ‘Umar bin Khatwwab (رضي الله عنه) - At-Tirmidhiy (1/78)  na taz Swahiyh At-Tirmidhiy (1/18)]

 

سُبْحـانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمدِك أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْك

SubhaanakaAllaahumma wabihamdika, ash-hadu an laa ilaaha illa Anta astaghfiruka wa atuwbu Ilayka

 

Kutakasika ni Kwako ee Allaah,  na Himdi ni Zako, nashuhudia (kwa kuamini moyoni na kukiri) kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, nakuomba unighufurie na natubia Kwako  

[Hadiyth ya Abu Sa’iyd Al-Khudriyy(رضي الله عنه)  -An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah’ (Uk. 173), (81) na taz  Irwaa al-Ghaliyl (1/135),  (3/94)] 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share