Hadiyth Dhaifu Jibriyl Kumwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kuwa Anaweza Kuhesabu Tone Za Mvua..

SWALI:

 

Malaika gibril alimtokea mtume Muhammad akamwambia kama ana uwezo wakuhesabu matonya ya mvua kipindi inanyesha ila hawezi kuhesabu madhambi ya watu wane. Ningependa munisadiye hao watu ni akina nani? Naomba munisaidiye kwa ushahidi wa qur'ani na Hadiyth za mtume.


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Jibriyl kumweleza hayo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Hakika ni kuwa hakuna Aayah ya Qur-aan inayozungumzia suala hilo. Na pia hatujapata Hadiyth sahihi yenye kutuelezea sisi kuhusu jambo hilo.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share