Mafunzo Gani Tunapata Katika Kisa Cha Asw-haabul Fiyl

SWALI:

 

Taja somo na mazingatio ambayo yanapatikana na kutokea tukio la tembo {as-habul-fiyl}, linaloendana na matukio ya ya zama hizi katika dola ya kitwaghut.


 

 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Masomo na mazingatio ambayo tunayapata katika kutokea tukio la tembo ni kuonyesha uwezo mkubwa wa Allaah Aliyetukuka. Hakuna nguvu kuu mbinguni wala ardhini inayolingana au kuzidi ile nguvu Yake. Na kuwa Allaah Aliyetukuka Anailinda Nyumba Yake kutokana na vitimbi na mikakati ya maadui wasiotaka nyumba hizo zisimame hapa duniani. Na pia kuwa Allaah Aliyetukuka Huwasaidia waja wake wema hata ikiwa ni wachache. Na katika wakati wa leo tunaona vipi Misikiti ya Allaah inavyohifadhiwa kwa njia moja au nyingine.

Pia mafundisho tunayopata ni kuwa upo uwezekano wa kuwavamia maadui kutoka angani kama walivyofanya ndege waliotumwa na Aliyetukuka. Na si kuvamia tu bali kurusha vitu, wakati huo ilikuwa ni vijiwe vilivyoweza kuwaua maadui kwa kufanya viungo kudondoka kimoja kimoja na wakawa kama majani yaliyotafunwa. Katika zama zetu, tumeona jinsi gani zinaweza kutumika njia mbalimbali za kupambana maadui wa mbali kwa silaha za kurushwa kwa masafa marefu na zikashuka katika eneo la adui na kuwaangamiza, kama ndugu zetu wa Palestina wanavyotengeneza mizinga ya masafa ya mbali na wakaweza kujihami nayo kwa maadui wao wa kizayuni ambao wanatumia silaha za kila aina na chafu zisizo halali hata katika sheria zao za silaha za kuwateketeza watoto na raia wasio na hatia. Hata hivyo pamoja na hayo, kama inavyotueleza Qur-aan na Hadiyth Sahihi za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) matwaghuti hawatoweza kubakia katika hali ya ushindi daima kwani wenye kunusuriwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ni Waumini.

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share