Zidisha Uzito Mizani Yako Siku Ya Qiyaamah

 

Zidisha Uzito Mizani Yako Siku Ya Qiyaamah

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

   

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

فَأَمَّا مَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ ﴿٦﴾

Basi yule itakayekuwa mizani yake nzito.

 

فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ ﴿٧﴾

Huyo atakuwa katika maisha ya kuridhisha. [Al-Qaari'ah:6-7]

 

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿١٠٢﴾

Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, hao ndio wenye kufaulu. [Al-Muuminuwn: 102]

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anatujulisha kwamba yule mwenye kuwa na mizani nzito ya ‘amali njema ndiye atakayekuwa na maisha mema ya kumridisha Siku ya Qiyaamah ambayo ni kuingizwa Peponi.

 

Kuifanya mizani yako iwe nzito kwa ‘amali njema ni ni kutenda yafuatayo:

 

1-Kufuata amri za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kujiepusha yote yaliyoharamishwa.

 

 

 

2-Baada ya kutimiza ipasavyo yaliyo ya fardhi, ni kutekeleza yaliyo ya Sunnah

 

Kama Swalaah za Sunnah, Swawm za Sunnah, kutekeleza ‘Umrah, kutoa swadaqah.

 

 

3-Kutenda mengineyo yaliyokuwajibika

 

Mfano kuwatendea ihsaan wazazi wawili, kuunga undugu, kuwatendea wema majirani, kulea yatima.

 

 

4-Kuzidisha wingi wa khayraat nyenginezo zisizoweza kuhesabika

 

Mfano kulisha masikini na mafukara, kusaidia wenye shida, kusaidia wagonjwa na kuwatembelea, kufanya swadaqatun-jaariyah kama kuchimba visima, kujenga Misikiti, kusaidia wanaotafuta elimu, kusoma Qur-aan kwa wingi, kuomba maghfirah na mengi mengineyo yenye sifa ya matendo mema.     

 

 

5-Kumsabbih Allaah ('Azza wa Jalla) kama ilivyotajwa katika Hadiyth:

 

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: " كَلِمَتَانِ خَفِيفَتَانِ عَلَى اللِّسَانِ، ثَقِيلَتَانِ فِي المِيزَانِ، حَبِيبَتَانِ إِلَى الرَّحْمَنِ: سُبْحَانَ اللَّهِ العَظِيمِ، سُبْحَانَ اللَّهِ وَبِحَمْدِهِ " رواه البخاري ومسلم

Imetoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema ((Maneno mawili ni mepesi mno juu ya ulimi, mazito mno katika mizani, yanapendeza mno mbele ya Ar-Rahmani (Mwenye kurehemu) nayo ni:

 

 

سُبْحانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ  سُبْحَانَ اللهِ العَظِيمِ

 “Ametakasika Allaah na Himdi ni Zake, Ametakasika Allaah Aliye Mtukufu” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

6-Kuwa na khulqah (tabia) njema.

 

Mwenye tabia njema atakuja kukuta mizani yake ya mema imekuwa nzito Siku ya Qiyaamah kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth ya  Abuu Dardaa (Radhwiya Allaahu 'anhu), kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna kitu kizito katika mizani ya Muumin siku ya Qiyaamah kuliko tabia njema. Hakika Allaah Humchukia mtu muovu mwenye tabia mbaya." [Imepokelewa na At-Tirmidhiy, na ni Hadiyth Hasan]

 

 

7-Kuomba Du’aa Ya Sunnah ifuatayo iliyotaja kuomba kujaaliwa mizani kuwa nzito:

 

 

أللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ خَيْرَ الْمَسْأَلَةِ، وَخَيْرَ الدُّعَاءِ، وَخَيْرَ النَّجَاحِ، وَخَيْرَ الْعَمَلِ، وَخَيْرَ الثَّوَابِ، وَخَيْرَ الْحَيَاةِ، وَخَيْرَ الْمَمَاتِ، وَثَبِّتْنِي، وَثَقِّلْ مَوَازِينِي، وَحَقِّقْ إِيمَانِي، وَارْفَعْ دَرَجَاتِي، وَتَقَبَّلْ صَلاَتِي، وَاغْفِرْ خَطِيئَتِي، وَأَسْأَلُكَ الدَّرَجَاتِ الْعُلَى مِنَ الْجَنَّةِ آمِينْ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ فَوَاتِحَ اْلخَيْرِ، وَخَوَاتِمَهُ، وَجَوَامِعَهُ، وَأَوَّلَهُ، وَآَخِرَهُ،  وَظَاهِرَهُ، وَ بَاطِنَهُ،  وَالدَّرَجَاتِ الْعُلىَ مِنَ الْجَنَّةِ آمِينْ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ خَيْرَ مَا آتِي، وَخَيْرَ مَا أَفْعَلُ، وَخَيْرَ مَا أَعْمَلُ، وَخَيْرَ مَا بَطَنَ، وَخَيْرَ مَا ظَهَرَ، وَالدَّرَجَاتِ الْعُلىَ مِنَ الْجَنَّةِ آمِينْ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ أَنْ تَرْفَعَ ذِكْرِي ، وَتَضَعَ وِزْرِي، وَتُصْلِحَ أَمْرِي، وَتُطَهِّرَ قَلْبِي، وَتُحَصِّنَ فَرْجِي، وَتُنَوِّرَ قَلْبِي ، وَتَغْفِرَ لِي ذَنْبِي، وَاَسْأَلُكَ الدَّرَجَاتِ الْعُلىَ مِنَ الْجَنَّةِ آمِينْ. اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ أَنْ تُبَارِكَ فَي نَفْسِي، وَفِي سَمْعِي، وَفِي بَصَرِي، وَفِي رُوحِي، وَفِي خَلْقِي، وَفِي خُلُقِي، وَفِي أَهْلِي، وَفِي مَحْيَايَ، وفي مَمَاتِي، وَفِي عَمَلِي، فَتَقَبَّلْ حَسَنَاتِي، وَاَسْأَلُكَ الدَّرَجَاتِ الْعُلىَ مِنَ الْجَنَّةِ آمِينْ.    

Ee Allaah hakika mimi nakuomba maombi bora kabisa na du’aa bora kabisa, na kufuzu bora kabisa, na ‘amali bora kabisa, thawabu bora kabisa, na uhai bora kabisa, na mauti bora kabisa, na nithibitishe, na fanya nzito Mizani yangu, na thibitisha iymaan yangu, na nyanyua daraja zangu, na Takabali Swalaah zangu, na Ghufuria madhambi yangu, na nakuomba daraja ya juu katika Jannah, Aamiyn. Ee Allaah hakika mimi nakuomba mwanzo mzuri, na khatima nzuri, na ujumla wa uzuri kutoka mwanzo mpaka mwisho wake, na dhahiri yake na undani wake, na daraja za juu katika Jannah, Aamiyn.

Ee Allaah hakika mimi nakuomba mazuri nnayoyaleta, na mazuri niyafanyayo, na mazuri niyatendayo, na mazuri yanayofichika, na mazuri yanayodhihiri, na daraja za juu katika Jannah, Aamiyn.

Ee Allaah hakika mimi nakuomba upandishe utajo wangu na uondoe dhambi zangu, na utengeneze mambo yangu, na utakase moyo wangu, na uhifadhi tupu zangu, na nawirisha moyo wangu, na unighufurie madhambi yangu, na nakuomba daraja za juu katika Jannah, Aamiyn.

Ee Allaah hakika mimi nakuomba unibariki katika nafsi yangu, na kusikia kwangu, na kuona kwangu, na roho yangu, na umbile langu, na tabia  yangu, na katika familia yangu, na katika uhai wangu, na katika mauti yangu, na katika ‘amali zangu, basi nitakabalie mazuri yangu, na nakuomba daraja za juu katika Jannah, Aamiyn. [Ameitoa Al-Haakim kutoka kwa Umm Salamah marfuw’ na ameipa daraja ya Swahiyh na ameikubali Adh-Dhahabiy (1/520)]

 

Hayo ni machache tuliyojaaliwa kuyataja kati ya mengi mengineyo yaliyothibiti katika Qur-aan na Sunnah ambayo yanafanya mizani ya Muuumin kuwa nzito.

 

Jambo muhimu baada ya hapo ni kuhifadhi hizo amali ili zisipotee bure akaja mtu Siku ya Qiyaamah akaona kwamba hana lolote jema alilolifanya. Na kuhifadhi huko ni kwa kuhakiksha Muislamu amehifadhi haki za Muislamu mwenzake. Yaani kutokumdhulumu mtu haki yake, kutokumsengenya nyuma yake, kutokumtukana mtu au kumuonea kwa njia yoyote kwani atakyefanya hivyo atakuta siku ya Qiyaamah mambo mema yote aliyotenda yamejazwa katika mizani ya yule aliyemdhulumu na yeye mizani yake ya mambo mema imekuwa aidha nyepesi au haina lolote. 

 

WabiLLaahi At-Tawfiyq

 

 

Share