Viazi Vya Kukaanga Na Sosi Ya Nyanya

Viazi Vya Kukaanga Na Sosi Ya Nyanya

 

 

 

Vipimo 

 

Viazi - 5 vya kiasi  

Bizari ya manjano - ½ kijiko cha chai 

Meti ya unga - ½ kijiko cha chai  

Mafuta - 2 kijiko cha supu  

Limro (majani ya kihindi) - 6 majani  

Nyanya - 1  

Pilipili mbichi - 3 

Ndimu - 1 

Chumvi - kiasi  

kidonge cha supu - ½  

Nyanya kopo au paprika - ½ kijiko chai  

Maji - ½ kikombe 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

  1. Katakata viazi virefu virefu kama uonavyo kwenye picha.
  2. Tiia mafuta kwenye sufuria, bizari ya manjano, meti, chumvi, kidonge cha supu na maji kisha funika na acha moto mdogo mpaka viive bila kukoroga.
  3. Tia nyanya, pilipili mbichi, nyanya ya kopo au paprika na ndimu, funika moto mdogo na huku unakoroga. kisha utaonja na itakuwa tayari kwa kuliwa.

 

 

Share