Namna Ya Kuiswali Swalah Ya Safari Ikiwa Kaipata Swalah Moja Kati Ya Mbili Za Kuunganisha

SWALI:

 

Assalaam Alaykum warahmatu Laahi Taala Wabarakatu, ama Baad.
Mashehe wetu wa Alhidaaya tunakutakieni kila la kheri na baraka, naomba muniiye radhi kwa maswali yangu yafuatao.


Jee naweza kusali salatu safar kama nasafiri hali yakua ile sala ya alasr sitoipata na kama inaruhusiwa naweza kusali rakaa mbili, yaani na sali rakaa 4 za zuhr na rakaa mbili ya alasr.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Swalah ya safari.

Swalah ya safari inaanza kuswaliwa baada ya kuwa ushaingia katika safari sio wakati umeweka Niyah ya kusafiri.

 

Ikiwa kwa sababu moja au nyingine uliswali Swalah kamili kwa mfano wakati wa adh-Dhuhr ikiwa hujaanza safari basi hiyo utaiswali kamili kabisa. Baada ya hapo ukianza safari na Swalah ya al-‘Asr ikikupata utaswali rakaa mbili ukiwa peke yako au ukiwa wewe ndiye Imaam. Ama ukiwa wewe ni maamuma unaswali nyuma ya Imaam ambaye ni mkaazi itabidi ukamilishe kwa kumfuata Imaam.

 

 

 

Mfano mwengine ni ikiwa uko safarini, ukaswali nyuma ya Imaam mkaazi Swalah ya adh-Dhuhr, pindi unapomaliza rakaa nne hizo utaswali rakaa mbili za al-‘Asr ukiwa peke yako au pamoja na jamaa na wasafiri wenzako.

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Kuswali Swalah Ya Safari Kwa Sababu Ya Umbali Wa Anapofanyia Kazi

 

Msafiri Anatambulikanaje Ni Msafiri Ili Afupishe Swalah na Swawm

 

Yupo Nje Masomoni Hapati Nafasi Ya Kuswali Chuoni, Aswali Swalah Ya Safari?

 

Kukidhi Swalah Ya Safari Na Namna Ya Kunuia

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share