Mkiristo Anataka Kujua Mipaka Ya Kumuona Mwanamke Wakati Anataka Kuchumbiwa

SWALI:

 

Kuna mkiristo mmoja aliniuliza suali juu ya namna ya ukomo wa namna unavyoweza kumchunguza mchumba unayetarajia kumuo kimaumbile. mwanzoni nikiwa peke yangu nilimjibu taratibu kuwa unaenda kwa wazazi wake na kumuona kwake kabla ya kumuoa ni kama anavyostahiki kumuona  mwanamke muislam wa kawaida na kwamba kabla ya kumuoa anpaswa kujiridhisha kwa umbile la nje na sikumuona sehemu ambazo zinakuwa ni uchi kwa mwanamke japo ni mchumba wake.

Siku nyingine mkristo huyo huyo alimuuliza muislam mwengine kutoka Nigeria naye alimwambia ikiwa kamchumbia anaruhusika kuona nywele zake na sehemu za viungo za mikono na miguu wakati akimjibu hayo nipo sikumpinga kwani sikuwa na elimu ya ufafanuzi wa hayo lakini bado nikawa nina wasiwasi juu ya hilo jibu hivyo naomba usahihi wa hili.

 

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mipaka ya kumuoana mchumba wako.

Kumuona msichana kabla ya harusi au Nikaah ni agizo la Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ili kupatikane mapenzi baina ya wanandoa hao wawili. Agizo hili limepuuzwa sana na Waislamu wa jinsia zote mbili wakiona kuwa hilo litaleta kuondoa baadhi ya ada kwa Waislamu wanaoishi katika sehemu tofauti duniani.

 

Agizo hilo la Mtume wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) lilitolewa kwa ujumla wake na hivyo kupokewa na Jaabir bin ‘Abdillaahi, Mughiyrah bin Shu‘bah na wengineo (Radhiya Allaahu ‘anhum), na kufanya hivyo ni kuleta upendo wa kuvutiana katika maumbile ya mwili ili kuweza kuoana (an-Nasaa’iy na Ibn Maajah). Na katika Hadiyth ya Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhuma) ni ya kijumla sana kwa kiasi ambacho wanachuoni wamesema mengi kuhusu jinsi ya kumuona msichana au mwanamke unayetaka kumuoa.

 

Kwa muhtasari ni kuwa mwanamme anaweza kumtazama msichana uso na mikono.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share