Supu Ya Koliflawa Viazi Na Parsley

 

Supu Ya Koliflawa Viazi  Na Parsley

 

Vipimo

 

 

 Koliflawa (cauliflower)  ½

 

Viazi 3

 

Kitunguu 1

 

Parsley kiasi

 

Siagi (butter)  - vijiko 2 vya kulia

 

Pilipili manga – ¼ kijiko cha chai

 

Supu ya kuku au kidonge cha supu – 1

 

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

 

  1. Katakata kauliflawa vipande vidogo vidogo.
  2. Menya viazi na katakata vipande vidogodogo.
  3. Weka siagi katika sufuria, tia kitunguu ulichokatakata kaanga kiasi tu kukaribia kulainika na kuanza kubadilika rangi.
  4. Tia koliflawa na viazi, chumvi, pilipili manga.
  5. Tia maji kiasi weka na kidonge cha supu au tumia supu ya kuku.
  6. Katia parsley au kotimiri, koleza chumvi na pilipili.
  7. Acha ichemke mpaka viwive viazi na koliflawa. Vikishawiva viazi na koliflawa, itie supu katika mashine ya kusagia usage kisha rudisha katika sufuria.
  8. Acha  katika moto kidogo kisha epua ikiwa tayari.

 

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

 

 

 

Share