Aayah Zipi Za Kusomwa Katika Swalaah Ya Sunnah Ya Alfajiri?

 Aayah Zipi Za Kusomwa Katika Swalaah Ya Sunnah Ya Alfajiri

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalaam alaykum Warahmatullah Wabarakatuh baada ya maamkizi hayo mema shukran zangu ziende kwa Mola wetu aliyetuumba Subhaana Wa Taala na pia alhidaaya. Sheikh nina maswali mengi kuhusu swala itakuwa vizuri kama utapata muda kunielimisha.

 

Naomba pia unipe ni aya ngapi alizokuwa akisoma Mtume Swalla Allah Alayhi Wa sallam katika suratul Baqarah na Ayah ngapi za sura Al Imran?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Zipo riwaayah kadhaa na tunadhani kuwa kuzieleza zote itawasaidia wengine pia. Miongoni mwazo ni:

 

1-Kusoma Al-Faatihah na Al-Kaafiruwn katika rakaa ya kwanza na Al-Faatihah na Al-Ikhlaasw katika rakaa ya pili [Hadiyth ya Abuu Hurayrah Radhwiya Allaahu ‘a hu katika Muslim].  

 

 

 

2-Kusoma Al-Faatihah na

 

قُولُوا آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَا أُوتِيَ النَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿١٣٦﴾

Semeni: Tumemwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na Al-Asbaatw na aliyopewa Muwsaa na ‘Iysaa na waliyopewa Manabii kutoka kwa Rabb wao, hatutofautishi baina ya mmoja yeyote miongoni nasi ni Waislamu (tunajisalimisha) Kwake. [Al-Baqarah: 136]

[Hadiyth ya Ibn ‘Abaas Radhwiya-Allaahu ‘ahumaa katika Muslim, An-Nasaaiy]

 

 

 

 

3-Kusoma Al-Faatihah na

 

 

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٦٤﴾

Sema: Enyi Ahlal-Kitaabi! Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu, kwamba tusiabudu isipokuwa Allaah Pekee, na wala tusimshirikishe na chochote, na wala wasichukue baadhi yetu wengine kuwa miola badala ya Allaah. Wakikengeuka; basi semeni: Shuhudieni kwamba sisi ni Waislamu. [Aal-‘Imraan: 64]

 

 

4-Na mara nyingine alikuwa akibadilisha Aayah ya Suwrah Aal-‘Imraan katika rakaa ya pili kwa kwa kusoma:

 

فَلَمَّا أَحَسَّ عِيسَىٰ مِنْهُمُ الْكُفْرَ قَالَ مَنْ أَنصَارِي إِلَى اللَّـهِ ۖ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ اللَّـهِ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَاشْهَدْ بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٥٢﴾

Basi alipohisi ‘Iysaa ukafiri kutoka kwao; alisema: Nani wanusuruji wangu kwa ajili ya Allaah? Wakasema wafuasi watiifu:  Sisi ni wasaidizi wa Allaah. Tumemwamini Allaah na shuhudia kwamba sisi ni Waislamu (tunajisalimisha Kwake). [Aal-‘Imraan: 52]

[Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas Radhwiya-Allaahu ‘anhumaa katika Muslim na Abuu Daawuwd]

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share