Du'aa za Qunuwt Ziko Ngapi Na Je Lazima Zisomwe Katika Swalaah Ya Alfajiri?

 

Du'aa za Qunuwt Ziko Ngapi Na Je Lazima Zisomwe Katika Swalaah Ya Alfajiri?

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Salam alaikum,

Mie swali langu ni kwamba dua hii ya Qunut ni lazima iombwe usiku baa ya kusali rakaa mbili au unaweza ukaomba wakati wowote?

Pia naomba unipatie dua yenyewe kama iko tofauti na ile isomwayo katika swala ya alfajir.

Ahsante.

 

 

JIBU: 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kwanza tujue kwamba maana ya 'Witr' (witiri) ni namba isiyoweza kugawanyika kama moja au tatu au tano na kadhalika. Na Swalaah ya Witr ambayo ni Sunnah iliyosisitizwa sana, huswaliwa usiku baada ya Swalaah ya 'Ishaa hadi asubuhi kabla ya Alfajiri. Hivyo hakuna Raka'ah mbili zinazoswaliwa usiku na kusomwa du'aa ya Qunuwt kama ulivyosema, bali husomwa du'aa hiyo baada ya kuinuka kutoka kurukuu katika Raka'ah ya mwisho ya Swalaah za Witr.

 

Unaweza kuswali Raka'a tatu au tano au saba au tisa au kumi na moja. Utaswali Raka'a mbili mbili na kila baada ya Raka'ah mbili utatoa Salaam kisha utamalizia na Raka'ah moja ndio utasoma hiyo du'aa ya Qunuwt baada ya kuinuka kutoka kurukuu. Na kama huna uwezo wa kuswali hivyo basi hata Raka'ah moja itakutosheleza kupata fadhila za Witr na kusoma du'aa ya Qunuwt kutokana na dalili ya Hadiyth ifuatayo:

   

((صلاة الليل مثنى مثنى فإذا خشيت الصبح أوتر بواحدة)) أخرجه البخاري

((Swalaah ya usiku ni (raka’ah) mbili mbili na ukiogopa kukukuta Asubuhi  basi Swali Witr  [Raka'ah] moja)) [ Al-Bukhaariy]

 

Tafadhali ingia katika viungo vifuatavyo upate faida ziyada kuhusu Swalaah ya Witr na Du'aa ya Qunuwt:

 

 

Je Ni Sunnah Kusoma Du'aa Ya Qunuwt Katika Swalaah Ya Alfajri

 

 

Suwrah Gani Kusoma Katika Swalaah Ya Tahajjud Na Witr?

 

 

Du'aa za Qunuwt zilizothibiti katika Sunnah zinapatikana katika viungo vifuatavyo ambapo mna uwezekano wa kusikiliza du’aa hizo pia:

 

 032-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Qunuwt Ya Witr

 

 

033-Hiswnul-Muslim: Du’aa Baada Ya Salaam Katika Swalaah Ya Witr

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share