Nyama Ya Mbuzi Ya Kukausha Na Viazi

Nyama Ya Mbuzi Ya Kukausha Na Viazi

 

Vipimo

  
Nyama ya mbuzi ilokatwa vipande - 4 Lb

Viazi vilivyomenywa na kukatwa - 4 

Tangawizi iliyosagwa - 1  Vijiko vya supu

Kitunguu saumu/thomu kilosagwa - 1 kijiko cha supu

Pilipili nyekundu  nzima - 3

Pilipili manga ya unga - 2 vijiko vya chai 

Mdalasini  - 1 kijiti

Jira (bizari ya pilau/cummin powder)  - 1 kijiko cha chai

ndimu  - 2-3 vijiko vya supu

Chumvi - kiasi

Kitunguu kilichokatwa - 1 kikubwa

Nyanya ilosagwa - 2 kijiko cha supu

Mafuta - ¼ kikombe  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika 

  1. Katika sufuria tia vijiko 3 mafuta, kisha tia nyama na pilipili manga, chumvi na mdalasini, na ikaange kidogo.
  2. Tia maji kiasi tu ya kuivia nyama, ichemshe hadi iwive. Ikiwa supu imebakia itoe weka kando.   .
  3. Menya viazi katakata vipande vya mraba, kanga weka kando.
  4. Katika karai, weka mafuta yaliyobakia tia vitunguu kaanga hadi vigeuke rangi. Tia nyama pamoja na viungo vyote, katika  pilipili mbichi kwa urefu,  kisha ikaange nyama hadi igeuke rangi kidogo. Unaweza kuongezea supu yake kidogo iwe na sosi.
  5. Tia viazi na changanya vizuri na tayari kupakuliwa 

Kidokezeo: Ukipenda unaweza kukatia mapilipili boga na karoti.

 

Share