Ameacha Watoto Wa Kiume Na Wakike Wakiwa Matumbo Mawili Tofauti – Mke Mkubwa Alimuacha Kabla Ya Kifo – Je Watoto Wake Wanahaki?

SWALI:

 

ASS-ALAM ALAIKUM?

Mtu amefariki ameacha watoto wa KIUUME/WAKIKE, wakiwa wamezaliwa ktk matumbo mawili tofauti, Mke mkubwa alisha muacha kabla ya kifo chake. Jee hawa watoto wa mke mkubwa wanawajibu wa kisheria wa kumtimizia mahitajio kizuka huyu? Naomba jibu kwa Qurani na Khadithi. WABILAHI TAWFIQI.

 


 

 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mirathi baada ya kufa baba mzazi. Katika Uislamu, watoto wa aliyefariki ni watoto, wawe ni wakike au wa kiume, wawe ni kutoka tumbo moja au kwa mama tofauti. Kila mmoja amepatiwa haki yake ya kurithi ya Allaah Aliyetukuka.

 

Baba anapofariki akiwa mke wake wa kwanza aliyemtaliki yu hai, mke huyo hatapata chochote katika mirathi. Mke mwenye kupata mirathi ni yule ambaye ni mke wa aliyefariki. Aliyefariki akiwa na watoto kama ilivyo katika swali lako, mke wa aliyefariki anapata thumuni (1/8). Hii ni kwa ajili ya maneno ya Aliyetukuka: “Na wake zenu watapata robo mlicho kiacha, ikiwa hamna mtoto. Mkiwa mna mtoto basi sehemu yao ni thumni ya mlicho kiacha, baada ya wasia mlio usia au kulipa deni” (an-Nisaa’ [4]: 12).

 

Na watoto wake wanapata kwa kiwango kifuatacho, kijana wa kiume sehemu mbili kwa msichana sehemu moja. Allaah Aliyetukuka Anasema: “Allaah Anakuusieni juu ya watoto wenu: Fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili” (an-Nisaa’ [4]: 11). Wale ambao hawatarithi ni watoto wa mke mkubwa aliyetalikiwa aliowapata kwa mume mwingine au watoto wa mke wa pili alionao kutoka kwa mume mwingine labda kabla hajaolewa na aliyefariki hata kama amewalea yeye, aliyefariki.

 

Ikiwa tutapata idadi ya watoto wa aliyefariki, wa kike na wa kiume tunaweza kuwajulisha kila mmoja atarithi ngapi.

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share