Ni Mfanyi Kazi Ambaye Kipato Chake Hakikidhi Mahitaji Yake, Afanyeje?

SWALI:

 

AsALAMU ALAYKUM

Mimi naitwa …………………….  Natokea TANZANIA (ZANZIBAR)

ombi langu ni kutaka kujua kama ni mimi ni mfanya kazi lakini kutokana na kazi nnayoifanaya mahitaji yangu binafsi kutokana na kiwango cha mshahara haukidhi ila nimeamua kufanya biashara ya ili pesa zanzu zikizi mahitajio yangu kwa hiyo naomba msaada wenu nifanyeje ili mungu na amimi aniinue kiuchumi ili nikidhi mimi na family fangu pia nisiweze kumshirikisha na jambo lolote lile lililo baya Sina la Ziada ila hayo tu ASALAMU ALAYKU WARAH-MATULLAHI WABARAKATU

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu pesa unazopata kwa kufanya hazikidhi mahitaji yako ya msingi. Ndugu yetu mpendwa, mas-ala haya ni mas-ala yaliyofungamana na mtihani ambao tunapatiwa hapa duniani na Allaah Aliyetukuka. Kipato anachopata mtu kinaweza kuwa kingi na huo ni mtihani na kinaweza kuwa kidogo na huo pia ni mtihani. Ndio Nabii Sulaymaan (‘Alayhis Salaam) akasema: “Haya ni katika fadhila zake Mola wangu Mlezi, ili Anijaribu nitashukuru au nitakufuru. Na mwenye kushukuru, kwa hakika, anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake; na anaye kufuru, kwa hakika Mola wangu Mlezi ni Mkwasi na Karimu” (an-Naml [27]: 40).

 

Mafanikio baada ya tawfiki ya Allaah Aliyetukuka hutegemea na juhudi ya mtu mwenyewe. Ikiwa umeweka azma ya kufanya biashara, biashara ni kazi moja ambayo ina baraka sana swali Swalaah ya Istikhaarah kumtaka shauri Allaah Aliyetukuka kama biashara hiyo ni muafaka au la.

 

Pindi unapoanza biashara mafanikio yatatokana na wewe kujiweka katika:

 

  1. Dini, ushikamane nayo barabara katika hali zote wala usiache Ibaadah zako kama Swalaah na nyinginezo.

 

  1. Uwe mkweli na mwaminifu katika kazi yote, hivyo usidanganye wala usisema uwongo.

 

  1. Usiwe ni mwenye kuapa yamini katika biashara na haswa yamini la uwongo kwani hilo litakuweka mahali pabaya.

 

  1. Na ikiwa utakuwa na mtu wa kukusaidia unatakiwa usimfanyie khiyana kabisa.

 

  1. Muombe Allaah Aliyetukuka sana katika nyakati ambazo du’aa inakubaliwa kama baina ya Adhana na Swalaah, unapoamka usiku wakati wa Tahajjud, unapofunga na kadhalika.

 

Na tunakuombea kwa Allaah Aliyetukuka Akufanyie sahali jambo hilo ulitakalo na liwe kheri kwako katika Dini yako, amali yako na hatima yako.

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share