Biashara Zipi Muislamu Anatakiwa Afanye

 SWALI:

Je ni ipi biashara ya muislamu nipe mifano na aina za biashara na pia nipe kulingana na sheria za kidini na mipaka yake. Allahu ahlam

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu biashara ambazo Waislamu wanaweza kufanya; yaani biashara zilizo halali.

Biashara zote ambazo zinafanywa kwa njia ya halali na mtu anauza cha halali basi ni halali kwake kufanya. Allaah Aliyetukuka Anasema:

Hayo ni kwa kuwa wamesema: Biashara ni kama riba. Lakini Allaah Ameihalalisha biashara na Ameiharimisha riba” (al-Baqarah 2: 275).

 

Mfano wa biashara ambazo ni halali ni kama:

 

1.     Kuwa na duka la kuuza matunda, nafaka na vyakula vinginevyo.

2.     Maduka ya kuuza nguo, viatu na kadhalika.

3.     Maduka ya kuuza vitabu vya Dini na masomo mengine yaliyo halali na mfano wake.

4.     Uuzaji wa nyama na maziwa ya wanyama walio halali, na kadhalika.

 

Kwa ufupi biashara yoyote ambayo hakujaingia riba wala kuuza vitu haramu kama nyama ya nguruwe na uuzaji wa pombe na mihadarati ni halali kwa Muislamu kufanya.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share