Fruti Kokteli Katika Rojo La Papai

Fruti Kokteli Katika Rojo La Papai

 

Vipimo: 

Papai - 1 kubwa

Maziwa - 2 Vikombe vya chai

Vanilla au ‘arki (rose essence) -  1/2 Kijiko cha chai   

Zabibu nyekundu -  2 Misongo (bunch)

Peya - 2                                                                     

Embe -  2

Nanasi -  ½  

Tikiti la asal (honey dew)  -  ½                                            

Ndizi -  2    

Sukari -  3 vijiko vya chakula                                                                                       

Namna Ya Kutayarisha:

  1. Katakata kila tunda vipande vidogodogo.
  2. Menya papai na saga kwenye mashine ya kusagia (blender) pamoja na maziwa, sukari na vanilla.
  3. Chukua bakuli  kubwa mimina  rojo la papai na maziwa changanya vizuri. 
  4. Mimina matunda yako uliyoyakata changanya na weka kwenye friji ipate baridi
  5. Ikishapata baridi vizuri itoe na tayari kwa kuliwa hasa baada ya chakula kama kitinda mlo.  

KIDOKEZO:

  1. Unaweza kuongeza matunda mengineyo au kubadilisha upendavyo.
  2. Utaangalia uzito wa rojo unaoutaka au unaweza kuongeza maziwa kiasi.
  3. Mchanganyiko huu ni mzuri kwa wale wenye matatizo ya tumbo (kutokupata choo)  
Share